Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi akiwata watanzania kuenzi vya kula vya asili,mila nzuri,desturi na lugha za asili kwa lengo la kutangaza utalii wa kiutamaduni wa taifa katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival leo jijini Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi akitizama namna maziwa yanahifadhiwa kwenye kibuyu na Bi Neema Mollel. Kutoka jamii ya Kimasai alipotembelea banda la wanawake kimasai wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival uliyofanyika leo jijini Arusha katika uwanja wa Shekhe Amri Abed.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi wapili kushoto akipata maelezo ya vyakula asili kwa Bi.Marium alipotembelea banda la kabila la Warangi leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abed jijini Arusha katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi wapili kushoto akipata maelezo ya vyakula asili kwa Bi.Marium alipotembelea banda la kabila la Warangi leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abed jijini Arusha katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival.
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (kushoto) akicheza ngoma ya asili ya Kimasai leo katika ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival katika uwanja wa Shekhe Amri Abed Mkoani Arusha anayecheza nae ni mmoja wa wacheza ngoma hiyo Bi. Neema Mollel baada ya kumaliza ukaguzi wa mabanda ya washiriki wa maonesho ya tamasha hilo.
Wacheza ngoma kutoka jamii ya Wasonjo Kutoka Ngorongoro wakicheza ngoma ya asili wakati wa ufunguzi wa Tamasha la Urithi Festival leo katika uwanja wa Shekhe Amri Abed Jijini Arusha ambapo mgeni rasmi wa ufunguzi wa tamasha hilo alikuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (hayupo pichani) .
Mama kutoka
jamii ya Kimeru Bi.Sophia Pallangyo akimwonyesha mgeni rasmi ambaye ni
Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni
Sanaa na Michezo Bi.Susan Mlawi (hayupo
pichani) namna jamii hiyo ilivyokuwa ikitumia mawe kusaga mahindi kupata unga
kama sehemu ya maonesho ya zana za asili,wakati mgeni rasmi alipombelea banda
hilo leo katika Maonesho ya washiriki wa
Tamasha la Urithi Festival linalofanyika uwanja wa Shekhe Amri Abed Jijini
Arusha.
Na Anitha Jonas –
WHUSM
09/10/2018
Arusha.
Serikali imewataka
watanzania kudumisha na kurithisha amali
za urithi wa asili wa utamaduni wa kitanzania kwa vijana na watoto kwa manufaa ya
kizazi kijacho.
Kauli hiyo imetolewa
leo jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Bi.
Susan Mlawi alipokuwa akifungua Tamasha la Urithi Festival kwa niaba ya Waziri
wa Habari Utamaduni Sanaa na Utamaduni Dkt. Harrison Mwakyembe katika uwanja wa
Shekhe Amri Abed.
Akiendelea kuzungumza
katika sherehe hizo za ufunguzi wa
Tamasha hilo Bi.Mlawi asisitiza kuwa uwepo wa tamasha hilo utatoa fursa
mbalimbali kwa watanzania wa kunadi,kuonesha na kutangaza rasilimali za utalii wa utamaduni ndani na nje ya nchi.
“Uanuai wa Maendeleo
ya sekta ya utalii wa kiutamaduni ili uishi na usiwe katika hatari ya kupotea unahitajika
kutambua na kuthamini urithi wa Jadi kama Mila,Desturi,Lugha,Maadii na Imani hivyo
uhifadhi,utafiti na utasaidia kunadi kutaendeleza rasilimali za asili za
taifa,”alisema Bi.Mlawi.
Kwa upande wa
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha la Urithi Festival Taifa Prof.Audax
Mabula alieleza kuwa wazo la kuanzishwa kwa tamasha hilo lilitokea Wizara ya
Maliasili na Utalii lengo likiwa ni kutangaza utalii wa kiutamaduni kwani
Tanzania imebarikiwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni ambavyo ni hazina
kuwa kwa Taifa.
“Nchi
yetu imebarikiwa kwa kuwa na vivutio vingi vya kiutamaduni kama michoro ya
mapangoni inayopatika kama Kondoa,makundi manne ya lugha za afrika
yanayopatikana mkoa wa Manyara na jirani,ngoma za asili kutoka makabila
mbalimbali nchini pamoja na vyakula vya asili,”alisema Prof.Mabula.
Aidha,
nae Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Usimamizi
wa Wanyapori Tanzania Dkt. James Wakibala
alitoa salamu za Waziri wa Maliasili Utamaduni Sanaa na Michezo kwa
wadau wa Mkoa wa Arusha na viongozi wake waliyoshiriki tamasha hilo kwa
kuwapongeza katika kushiriki tamasha hilo ambalo kwa namna moja litasaidia
kuendeleza utalii katika sekta ya Utamaduni.
Hata
hIvyo Katibu Mkuu huyo katika hitimisho la hotuba yake aliiomba Wizara hiyo ya
Maliasili na Utalii kushirikiana na Wizara yake katika maandalizi ya tamasha
hilo kwa mwakani kwani wote wanadhamana ya kukuza na kutangaza utalii wa Kiutamaduni.
Halikadhali
hitimisho la Tamasha hilo kwa mwaka huu linatarajiwa kufanyika Oktoba 13,mkoani
hapo na Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.