Katika mazungumzo hayo aliambatana na Katibu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi Ndg Hassan Bomboko, Katibu wa Idara ya Vyuo na Vyuo Vikuu Ndg Kaman Juma Simba, Katibu wa Idara ya Usalama na Maadili Ndg Mohamed Abdalla na maafisa wawili kutoka Makao Makuu.
Ndugu Ngemela Lubinga aliwaasa Makatibu wa Idara za UVCCM Makao Makuu kuwa wabunifu na Wachapakazi ili kuleta mabadiliko Chanya hasa kwa Vijana wa Taifa letu, pia alisisitiza kuwa waadilifu, wamoja, waaminifu, wenye upendo na watiifu wakati wote. Pia aliongeza ya kwamba Taifa la kesho linajengwa leo na wakuifanya kazi hiyo ni sisi vijana.
Aidha, Ndugu Lubinga aliahidi ushirikiano mkubwa kwa sisi vijana kwenye mambo yanayolenga ya Idara anayoiongoza.
Msafara wa UVCCM ulimshukuru Ndugu Ngemela Lubinga kwa kutenga muda kuzungumza nao na waliahidi kufanya kazi kwa bidii na utii mkubwa wakilenga kushughulika na masuala ya vijana nchi nzima.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.