GSENGOtV
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiongoza zoezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida, Wengine pichani ni Waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa, na Naibu waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega. (Picha Na Mathias Canal, WK)
Sehemu ya waombolezaji walioshiriki kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akizungumza wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) akiwa na Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji wakati wa kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi Mathew Mtigumwe akitoa taarifa za miili ya marehemu wakati wa zoaezi la kuaga miili ya watumishi watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba 2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na rasilimali watu Bi Hilda Kinanga akieleza hatua zilizochukuliwa na wizara ya kilimo tangu kutokea ajali iliyoua watumishi watano wa wizara hiyo katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida.
Na Mathias Canal-WK, Dodoma
Waziri wa kilimo Mhandisi Dkt Charles Tizeba (Mb) leo Jumanne
tarehe 23 Octoba 2018 ameongoza mamia ya waombolezaji kuaga miili ya watumishi
watano wa wizara ya kilimo waliofariki kwa ajali ya gari juzi tarehe 21 Octoba
2018 katika kijiji cha Njiri Wilaya ya Manyoni Mkoani Singida wakiwa safarini
kutokea Jijini Dodoma kuelekea mkoani Shinyanga na Mwanza kikazi.
Ajali hiyo iliyolihusisha Lori la mizigo na gari ya serikali
STK 8925 iliyokuwa na watumishi hao watano ambao walikuwa safarini kuungana na
Ujumbe wa Benki ya Maendeleo ya afrika (AFDB)
kwa maandalizi ya utekelezaji wa mradi wa kuanzisha viwanda vya kusindika mazao
(Stage Agro Processing Zone).
Dkt Tizeba amelitaka jeshi la Polisi Mkoa wa Singida kutoa
taarifa zilizo sahihi tofauti na taarifa walizozitoa awali za ajali hiyo kwani
zinakinzana na maelezo ya dereva wa Lori ambaye amelazwa katika Hospitali ya
Wilaya ya Manyoni vilevile kukinzana na maelezo yanayotolewa na mashuhuda waliopo
katika eneo la ajali hiyo.
“Naomba Kauli iliyotolewa na jeshi la polisi irudiwe tena
waende wakafanye utafiti wa kweli kwani kumekuwa na lawama kwa dereva wa
serikali ambazo hazistahili maana taarifa zinasema kuwa dereva wa Lori alikuwa
anaingia barabarani pasina kufuata taratibu jambo lililopelekea kutokea kwa
ajali hiyo”
“Ninaomba sana jeshi la polisi kutenda haki katika tukio hili
lenye kuacha maumivu kwa familia, wizara na Taifa zima” Alikaririwa Dkt Tizeba
Waziri Tizeba amewataka wananchi kuacha kulaumu na kutoa
hukumu kwa dereva wa serikali kwa kusababisha ajali hiyo badala yake kuwaombea
marehemu wapumzike kwa amani kwani hakuna binadamu anayeweza kusababisha ajali
na vifo vya watu wengi kwa makusudi.
Watumishi hao walioagwa kwa kupoteza maisha kwa ajali ya gari
ni Dereva Mwandamizi wa wizara ya kilimo Ndg Abdallah Seleman Mushumbusi (53), Afisa
kilimo wa Wizara Ndg Charles Joseph Somi (33), Mkemia daraja kwanza Ndg Erasto
Isack Mhina (43), Mtakwimu daraja la kwanza Bi Ester Tadayo Mutatembwa (36) na
Mhasibu daraja la pili Bi Stella Joram Ossano (39).
Aidha, Mhandisi Tizeba ametoa pole kwa familia, ndugu, jamaa,
marafiki na watumishi wote wa wizara ya kilimo kwa kupoteza nguvu kazi ya Taifa
tena watumishi hao wakiwa safarini kutekeleza majukumu ya kiserikali.
Vilevile amewashukuru wabunge wa kamati ya kudumu ya maji,
kilimo na mifugo kwa kuacha kikao kazi ili kuungana na waombolezaji kuaga miili
ya watumishi hao.
Viongozi wengine walioshiriki katika zoezi la kuaga miili
hiyo ni pamoja na waziri wa fedha na Mipango Mhe Philiph Mpango, Waziri wa Viwanda, Bishara na Uwekezaji Mhe Charles Mwijage, Naibu waziri
wa Mifugo na Uvuvi Mhe Abdallah Ulega na Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa
na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya kilimo Prof Siza Tumbo.
Kwa upande wake katibu Mkuu wa wizara ya kilimo Mhandisi
Mathew Mtigumwe amewataja watumishi hao waliofariki kuwa walikuwa wachapakazi
hodari, wapole, wacheshi na waadilifu hivyo kufuatia mauti iliyowakumba Wizara
imepata pengo kubwa.
Alisema kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma mwajiri
anagharamia misiba hiyo na kuahidi kushirikiana na ndugu wa marehemu kwa ajili
ya taratibu nyingine za kupata haki na mafao yao.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.