Mkutano wa Afrika wa Azaki (CSOs) unafanyika mji wa Bajul Gambia ukiwa na lengo la kutathimini utekelezaji wa maazimio ya Tume ya Afrika juu ya kulinda haki za binadamu Afrika, Mkutano huo umendaliwa na kamisheni ya Afrika inayoshughulika na haki za binadamu.
Mkutano huo ulichagizwa na uwasilishwaji wa mada mbalimbali kama kutathimin demokrasia na haki za binadamu Afrika, utawala wa sheria katika bara la Afrika, tathimini ya mkataba wa Maputo wa kulinda haki za wanawake na watoto, rushwa na athari zake katika jamiii. Onesmo Olengulumwa Mratibu wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania, amesema kuwa, Tanzania imeonekana kufanya vizuri kwenye eneo la kupambana na rushwa, kwani Rais Magufuli mekuwa mstari wa mbele kwenye kuchukua hatua za kupiga vita rushwa na kuwepo kwa usawa katika jamii.
Ameongeza kuwa, changamoto zimebaki kwenye maeneo machache kama, haki za kisiasa, uhuru wa kujieleza, uhuru wa vyombo vya bahari, ambapo kimsingi azaki zina nafasi ya kuzidi kuishauri serikali juu ya hali hiyo.
Suala la uwepo wa rushwa limeonekana kuwavuta washiriki wengi kuchangia na kuitaka kamisheni kamisheni ya Afrika ya haki za watu kutafuta njia ya kuzihusisha serikali za Afrika kuchukua hatua kali za kudhibiti rushwa. Hasa kwa Nchi ambazo zilisaini mkataba wa kupambana na rushwa lakini ndio zinaongozwa kwa vitendo vya rushwa barani Afrika
Bi Christina Kamili Mkurugenzi wa Mtandao wa wa Mashirika yanayotoa Huduma ya Msaada wa Kisheria alisema kuwa, hakuna maendeleo bila haki na amani, hivyo serikali za Afrrika zifanye jitihada za kuhakikisha kuwa kila Mwananchi anapata msaada wa kisheria na pia zijengwe taasisi imara zitakozozingatia usawa katika upatikanaji wa haki.
Aliongeza kuwa, Serikali lazima zitenge bajeti na kuzijengea uwezo taasisi zinazotoa haki katika kuhakikisha kwamba jamii iliyopo pembezoni na watu maskini wanapata haki.
Naye Harusi Mpatani Mkurugenzi wa Kituo cha Huduma za Sheria Zanzibar alisema kuwa, uwepo wa kamisheni ya Afrika ya haki za watu isistize Nchi wanachama wanalinda na kutetea haki za binadamu pamoja na kuwepo mikakati thabiti ya kulinda taasisi za ndani zinazosimamia haki za binadamu, pia ametoa ushauri kwa mheshimwa Rais John Pombe Magufuli kuharakisha mchakato wa kupatikana kwa makamishina wa haki za binadamu, ambao ni kiungo muhimu katika kusimamia masuala ya haki za binadamu Tanzania.
Licha ya changamoto zilizopo katika kukabiliana na vitendo vya rushwa lakini kuna baadhi ya Nchi zimeonesha mfano mzuri wa kupambana na Rushwa, moja ya Nchi hizo ni Tanzania, ambayo imeanzisha mahakama maalumu ya kupambana na vitendo vya rushwa.
Mkutano huo wa siku tatu ulishirikisha mataifa yote ya bara la Afrika na washiriki zaidi ya 500 utamalizika leo Katika mji wa Banjul na kufanya mwendelezo wa mkutano mwingine hapo kesho wa vikao vya Kamisheni ya Afrika yenye makao yake makuu hapa Banjul Gambia utakaolenga kutathimini mwenendo wa haki za binadamu na utawala wa sheria Afrika.
Edwin Soko
Banjul
Gambia
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.