ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 16, 2018

YANGA HII SI YAMCHEZO, NGASSA APIGA BAO LAKE LA KWANZA.




HATRICK ya mkali wa Stand United, Alex Kitenge haikuwasaidia wapiga debe hao wa Shinyanga kuondoka na pointi tatu baada ya kukubali kichapo cha magoli 4-3 mbele ya wenyeji wao, Yanga SC katika mchezo uliopigwa kwenye dimba la Taifa.

Wakati Kitenge akifunga magoli matatu peke yake, Mrisho Ngasa alifunga goli lake la kwanza tangu ajiunge na Yanga kwa mara nyingine msimu huu huku magoli mengine yakifungwa na Vicent Andrew, Ibrahim Ajib na kiungo Deus Kaseke.

Ushindi huo wa Yanga unawafanya kufikisha jumla ya alama 6 sawa na Stand United United iliyopoteza.

Wakati huo huo Mbeya City iliyokuwa Uwanja wake wa nyumbani ikicheza na Alliance School ya Mwanza imefanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.