ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, September 16, 2018

CHADEMA CHALI, CCM YAZOA KATA ZOTE TATU.

Chama cha Mapinduzi kimefanikiwa kuibuka na ushindi katika kata tatu ambazo kura zake zimeshahesabiwa kwenye uchaguzi mdogo unaoendelea hivi sasa nchini.

Robson Kimarowa wa CCM ametangazwa kuwa diwani wa kata ya Machame Uroki baada ya kupata kura 2,174 dhidi ya kura 704 za mgombea wa Chadema.

Kutoka kata ya Maanga jijini Mbeya, Newton Mwajutobe wa CCM ametangazwa mshindi kwa kupata kura 1,897 dhidi ya kura 1,703 alizopata Mwashilindi ambaye ni mgombea wa Chadema.

Matokeo mengine  Yohana Laizer wa CCM ameshinda kata ya KIA mkoani Kilimanjaro kwa kujinyakulia kura 1,367 dhidi ya mgombea wa Chadema aliyepata kura 203

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.