ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 11, 2018

SERIKALI YATATUA ADHA YA USAFIRI KWA MAAFISA ELIMU KATA MKOANI MWANZA.

NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
JUMATATU ya September 10, 2018, Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI imekabidhi jumla ya pikipiki 189 kwa Maafisa Elimu Kata mkoani Mwanza ili kuwaondolea adha ya usafiri na kuongeza ufanisi na kuwarahisishia utendaji kazi wao.
Mkuu wa Mkoa Mwanza Mhe. John Mongella ndiye aliyesimamia zoezi hilo la makabidhiano ambapo Maafisa Elimu katika Kata zote 18 wamekabidhiwa vyombo vyao vya usafiri huku amewahimiza kuzitumia vyema ili kufikia malengo yaliyokusudiwa ya kurahisisha utendaji kazi wao. 
Kwa mujibu wa kaimu Afisa Elimu Jijini hapa Philipo Mukama amesema pikipiki hizo zimetolewa kupitia program ya EQUIP na LANES na thamani yake ni zaidi ya shilingi milioni 500 za kitanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.