ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 11, 2018

KOFFI ANNAN KUZIKWA ALHAMISI NCHINI GHANA.

MWILI wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan, ambaye alifariki mwezi uliopita, umewasili katika nchi aliyozaliwa, Ghana ukiwa umesitiriwa kwenye jeneza lenye bendera ya UN.

Mwili wake uliwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kotoka International Airport mjini Accra, ukisindikizwa na familia yake na maafisa wengine wa Umoja wa Mataifa.

Anatarajiwa kuzikwa kitaifa siku ya Alhamisi.
Askari wa Ghana wakilivisha bendera ya taifa jeneza la Kofi Atta Annan hatua chache baada ya kuupokea mwili huo katika uwanja wa Kotoka International Airport mjini Accra  September 10, 2018. [Picha na AFP]
 Kulikuwa na hali ya maombolezowakati mwili wake ukiwasili uwanjani hapo na kupokelewa na Rais wa Ghana Akufo Addo na viongozi wa kimila na kwa heshima ya kijeshi.

Mwili wake umehifadhiwa katika Ukumbi wa Kimataifa wa mikutano wa Ghana, wakati ukisubiri kuzikwa.
Askari wa Ghana, wakiwa wakiongozana na viongozi wa dini kwenye msafara wa kuupokea mwili wa aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa na kumalizia muda wake Kofi Annan. 
Kofi Annan alikuwa ni Katibu mkuu wa kwanza wa Umoja wa Mataifa, kutoka katika eneo la kusini mwa jangwa la Sahara na kuleta mafanikio sio tu katika bara la Afrika, lakini pia dunia nzima.

Aliwahamasisha vijana wengi nchini mwake na waliheshimu kile alichosimamia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.