NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Jeshi la polisi mkoani Mwanza limetoa onyo kali kwa askari wake na raia kutojihusisha na vitendo vya rushwa na kuwataka askari kufanya kazi kwa waledi kuacha kuwabambikizia kesi watu wasio na makosa kwa kuwaweka mahabusu kwenye vituo vya polisi.
Hayo yametolewa leo na Kamanda wa Polisi mkoani hapa Kamishna msaidizi wa jeshi la Polisi Jonathan Shanna wakati akizungumza na maofisa wa ukaguzi na askari wenye vyeo mbalimbali wakati wa kikao cha kazi kilichofanyika katika Bwalo la Polisi Mabatini jijini hapa.
Kamanda Shanna amekemea tabia ya baadhi ya askari kuomba na kupokea rushwa huku akiwanyoshea vidole raia wanaowashawishi kwa kutoa rushwa huku akiongeza kuwa mikakati mathubuti imewekwa ambapo atakayebainika kujihuusisha na vitendo hivyo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.
Ameongeza kuwa atakagua mahabusu zote zilizopo katika vituo vya polisi ili kubaini kama kuna watu wamebambikiwa kesi ili achukue hatua stahiki za kisheria. Aidha katika hatua nyingine ametangaza kufanya msako mkali dhidi ya Waganga wa jadi wanaojihusisha na upigaji ramli chonganishi zinazopelekea mauaji yatokanayo na imani za kishirikina.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.