ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 24, 2018

JPM AONGEZA MILIONI MOJA KWA WAFIWA NA WALIONUSURIKA AJALI YA MV NYERERE.

Rais Dk John Magufuli ameagiza kuongezewa kwa kiasi cha fedha shilingi milioni moja kwa kila familia iliyopatwa na msiba na watu 41 walionusurika katika ajali ya MV Nyerere iliyotokea Septemba 20, Mwaka huu katika Kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe Mkoani Mwanza.

Akizungumza na wananchi wa Ukara wilayani Ukerewe mkoani hapa, Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe amesema kuwa Rais Magufuli amemuagiza kuwapa taarifa kwa waliopoteza ndugu zao kuwa wataongezewa kiasi cha pesa cha shilingi milioni moja kutokana na kuguswa na tukio hilo.

Katika taarifa hiyo Kamwelwe amesema kuwa, fedha hizo zitaanza kutolewa hapo kesho Septemba 25, Mwaka huu kwa aliyenusurika na ajali hiyo pamoja na familia iliyopoteza ndugu yao ambapo fedha iliyopo hadi sasa ni shilingi milioni 39,720,000/=.

Aidha Waziri Kamwelwe amemuomba Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Venance Mabeyo kupeleka mafundi kwenda kukagua Meli ya MV TEMESA kama inakidhi kiwango ili iletwe hapa Ukara na  kufanya kazi kuanzia  Septemba 26, Mwaka huu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.