ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, September 24, 2018

MAJALIWA AWATOA HOFU WATANZANIA KUHUSU FEDHA ZA RAMBIRAMBI MV NYERERE.

 Siku moja baada ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuongoza mazishi ya kitaifa ya watu waliopoteza maisha kwenye ajali ya kuzama kwa kivuko cha MV Nyerere, leo ametoa ufafanuzi wa jinsi fedha za rambirambi zitakavyowafikia walengwa.

Serikali kupitia kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge, Kazi, Ajira na Watu wenye ulemavu) Jenista Mhagama ilitangaza akaunti maalumu iliyopewa jina la 'Maafa Mv Nyerere' namba 31110057256 tawi la Benki ya NMB Kenyatta jijini Mwanza ambapo watu walioguswa na msiba huo wa kitaifa wangeweza kuchangia chochote walichojaliwa.

Akizungumza leo na wananchi wa eneo la Ukara yalipotokea maafa hayo, Majaliwa amesema fedha zote za rambirambi zilizopatikana kutokana na kuchangwa na watanzania mbalimbali zitawafikia waathirika wa maafa hayo kupitia kwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.

Majaliwa aliwatoa hofu watanzania waliokuwa na hofu na matumizi ya fedha hizo ambazo kiasi cha Sh 300 Milioni kinatajwa kuchangwa mpaka sasa ambapo amesema fedha zote zitaelekezwa kwa wafiwa na waathirika kama ilivyokusudiwa.









Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.