ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 15, 2018

SERIKALI YAKABIDHI BOTI YA DORIA NA KITUO CHA POLISI WILAYANI CHATO

 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia), akiwaongoza viongozi wengine kutembelea eneo la mwambao wa Ziwa Victoria  baada ya kuikabidhi boti hiyo ya doria kwa Jeshi la Polisi, kutoka kushoto ni Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla, Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel na Diwani wa Chato, Richard BagolelePicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, Daniel Shilla akimshukuru Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni baada ya kumkabidhi Kituo cha Polisi kinachohamishika wilayani Chato. Katikatini Mkuuwa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masau ni (aliyeshika koti), akishuka katika boti maalumu aliyo wakabidhi Kikosi cha Polisi wilayani Chato ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchini. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi
Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Gabriel, akishuka katika boti maalumu iliyokabidhiwa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (hayupo pichani) kwa Kikosi cha Polisi Wanamaji wilayani Chato, ikiwa ni mkakati wa Serikali kupambana na uhalifu katika ukanda wa Ziwa na Bahari nchiniPicha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

SERIKALI kudhibiti Uhalifu Ukanda wa Ziwa na Bahari Na Mwandishi Wetu Serikali imejipanga kuimarisha Ulinzi na Usalama katika Ukanda waZiwa na Bahari kote nchini ili kuweza kudhibiti uhalifu unao tekelezwa majini   ikiwepo   uvuvi   haramu,   usafirishaji   wa   magendo   na   uhalifu mwingine unaotokea katika maeneo ya ziwa na bahari.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya boti maalumu ya doria naufunguzi wa Kituo cha Polisi Wanamaji, wilayani Chato, Naibu Waziriwa   Mambo   ya   Ndani   ya   Nchi,   Mhandisi   Hamad   Masauni   amesema lengo la Serikali ya Awamu ya Tano ni kuhakikisha inadhibiti uhalifu katika Ukanda wa Ziwa na Bahari kwa kutumia Vyombo vya Ulinzi na Usalama   vilivyopo   chini   ya   serikali,   ili   kuhakikisha   wananchi wanafanya   shughuli   za   kuchumi   bila   ya   kuwa   na   wasiwasi   juu   ya usalama wao 

Alisema  moja   ya  changamoto  kubwa aliyoelezwa   wakati alivyofanyaziara ya awali wilayani Chato ni kuwepo kwa matukio ya uhalifu ziwani yaliyo pelekea baadhi ya wananchi kusitisha shughuli za kiuchumi katika mwambao huo wa Ziwa Victoria.

“Serikali   ya   Awamu   ya   Tano   imedhamiria   kuleta   maendeleo   katika nyanja   zote   na   kuwawekea   mazingira   mazuri   wananchi   wake kujishughulisha   na   shughuli   za   kiuchumi,   hivyo   basi   tutahakikisha tunaimarisha   ulinzi  katika  sehemu  zote  ambazo  wananchi  wana fanya shughuli zao ikiwepo ukanda wa ziwa na bahari na leo hii tunaanzia hapa wilayani Chato. 

“Pia   nawasihi   askari   polisi   kufanya   kazi   kwa   maadili   na   agizo   hili nalitoa kwa nchi nzima na serikali kupitia Wizara ya Mambo ya Ndaniya Nchi aitomvumilia askari yoyote atakae bainika kuwabambikia kesi wananchi, hatua kali zitachukuliwa kwa atakae bainika” alisema Masauni ambae pia ni Mbunge wa Kikwajuni

Naye   Diwani   wa   Kata   ya   Muungano,   wilayani   Chato, Johnson Kilimo kwanza   alisema   anaishukuru   serikali   kwa   kuleta   boti   hiyo   naufunguzi   wa   kituo   cha   polisi   kwani   moja   ya   changamoto   iliyokuwa inawasumbua   wavuvi   katika   mwambao   huo   ni   masuala   ya   uhalifu unao tokea ziwani huku akiweka wazi uwepo wa kituo na boti ya doriavitapunguza masuala ya uhalifu.

Mmoja wa askari polisi ambae hakupenda  jina lake litajwe  alisema waowa naishukuru   serikali   kwa   kuwaletea   boti   na     kituo   ambavyo vitawa rahisishia kupambana na uhalifu “Muhimu naomba serikali pia waweze kutuletea gari ambalo litasaidiapia   katika   mapambano   hayo   ya   uhalifu   kama   unavyoona   tayari   tuna kituo   hapa   cha   wanamaji   naibu   waziri   amekizindua, muhimu   sasa tuletewe   usafiri   utakao wezesha   kupeleka   mahabusu   mahakamani,”alisema askari polisi huyo

IMEANDALIWA NA KITENGO CHA MAWASILIANO SERIKALINI-WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI

.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.