Kwa niaba ya MH, MBUNGE WA JIMBO LA ILEMELA MGENI RASMI Katibu wa Siasa na Uenezi CHIEF DENNIS LEKELA KANKONO amempongeza Mh, Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Makazi DR. ANGELINE MABULA kwa kuanzisha mashindano hayo kila mwaka na yameleta mafanikio makubwa na kuibua vipaji vya Vijana katika soka na wengine kusajiliwa katika timu za Mbao n.k.
Pia Katibu huyo amewaomba wadau na Wananchi kumuunga mkono Mh, Mbunge wa Ilemela katika shughuli mbali mbali za kuleta maendeleo katika Jimbo Ilemela sababu Michezo ni Afya na Ajira!! Mashindano hayo yako katika atua za Makundi ambapo bingwa atanyakua kitita cha sh.milioni _mbili, mshindi wa pili_ sh. milioni moja na nusu na mshindi wa tatu sh. milioni moja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.