ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, August 27, 2018

IJUE VYEMA HISTORIA YA GWIJI LA SIASA ZA MAREKANI NA MPINZANI WA OBAMA ALIYETANGULIA MBELE ZA HAKI.

John McCain alikuwa ni shujaa wa vita vya Vietnam ambaye alikuwa mwanasiasa aliyeheshimika sana nchini Marekani.

Ni mwanasiasa mwenye msimamo mkali ambaye mara nyinyi alikuwa anatofautiana na wanachama wenzake wa Republican na alikuwa mkosoaji mkubwa wa utawala wake Rais Donald Trump

Alishindwa kwenye uchaguzi wa mwaka 2008 huku akilaumiwa kwa uamuzi aliofanya wa kumteua Gavana wa Alaska Sara Palin kuwa mgombea mwenza.

Seneta maarufu wa Marekani, John McCain, aliaga dunia Jumamosi akiwa na umri wa miaka 81.

McCain ambaye alikuwa anaugua saratani ya ubongo, alifariki katika chumba chake cha mapumziko mjini Sedona, Arizona, akiwa amezungukwa na familia yake.
Mwanasiasa huyo mkongwe aligunduliwa kuwa na ugonjwa huo hatari mnamo mwezi Julai mwaka 2017.
Famila ya McCain ilitangaza Ijumaa kwamba alikuwa amesitisha tiba "kwa sababu saratani imeenea sana."
Hadi kifo chake, McCain alikuwa anawakilisha jimbo la Arizona katika seneti ya Marekani.
Baba yake na babu wote walikuwa ni wanajeshi
John Sidney McCain III Alizaliwa Agosti 29 mwaka 1936 kwenye kambi ya jeshi huko Coco Solo panama, eneo ambalo wakati huo lilikuwa chini ya udhibiti wa Marekani. Taaluma ya kijenshi ilikuwa tayari kwenye damu yake kwa sanbabu baba yake na babu wote walihumu kama wanajeshi na hata wakashika nyadhifa za juu.


Mwana wa afisa mwandamizi katika jeshi la majini, Bw McCain alihitimu kutoka chuo cha jeshi la majini mwaka 1958 na alianza kazi ya urubani wa jeshi akiwa na umri wa miaka 22.

Akapelekwa vitani nchini Vietnam, alinusurika kifo Julai ya mwaka 1967, wakati alipokuwa akijiandaa kwenda kufanya shambulio la anga, kombora liligonga matanki ya mafuta, hali iliyosababisha moto kwenye meli na watu 134 walipoteza maisha.

Miezi mitatu baadaye alitunguliwa kaskazini mwa Vietnam. Akakamatwa na wapiganaji wa Vietnam, alikataa kuachiliwa mapema.

Badala yake, alishikiliwa kama mfungwa wa kivita kwa zaidi ya miaka mitano, mahali alikokuwa akipigwa mara kwa mara na kuteswa hali iliyosababisha matatizo katika mikono yake.

Baada ya kurejea Marekani aliendelea kutumikia jeshi, hatimaye akawa mwambata wa jeshi la majini kwenye baraza la Seneti mpaka aliposataafu mwaka 1981.

Maisha ya kisiasa
Ilikuwa ni wakati huu ndipo alipohamia Arizona kujijenga katika maisha ya kisiasa, alifanikiwa kushinda uchaguzi wa Seneti mwaka 1982.

Akigombea dhidi ya George W Bush mwaka 2000 kuwania uteuzi wa chama cha Republican, Bw McCain awali alipata kuungwa mkono na kufanikiwa kushinda kura za maoni katika jimbo la New Hampshire.


Lakini alikabiliwa na upinzani mkali, akishambuliwa katika kampeni kwa kuchafuliwa, na hatimaye akahitilafiana na wajumbe wenye ushawishi mkubwa ndani ya chama wanaoegemea zaidi kwenye dini.

Alilizimika kuondoka kwenye uteuzi wa kuwania urais katika chama cha Republican mwaka 200
Bw Bush alisonga mbele kwa kushinda uteuzi wa chama cha Republican na McCain akarejea kwenye baraza la Seneti, akitumikia katika kamati muhimu ya maswala ya jeshi.

Bw McCain tangu wakati huo ameongeza msimamo mkali kuhusu baadhi ya maoni yake kama utoaji mimba, lakini bado haiminiki kikamilifu miongoni mwa wainjilisti kuwa yeye anafuata misingi ya kidini kama wao.

Licha ya kuahidi kumuunga mkono Bush, alionyesha wazi kuwa hakuwa na hofu ya kumkosoa rais mpya. Alikuwa mmoja wa maseneta wawili wa Republican waliopiga kura kupinga kupunguzwa kodi na kuping sera za rais kuhusu kudhibiti bunduki.

Baada ya mashmbulizi ya Septemba 11 aliunga mkono vita vya George Bush nchini Afghanistan, lakini baadaye aliweza kuhoji kuhusu mikakati ya Bush na sera za waziri wa ulinzi Donald Rumsfeld.

Matokeo mabaya
Mwezi Aprili mwaka 2005 McCain tena alitangaza kuwa angewania uraia ambapo alipambana na washindani wawili kutoka kwa meya wa Nee York Rudy Giulani na meya wa Massachusetts Mitt Romney katika uteuzi wa Republican.

Hata hivyo alishangaza kila mtu kwa kumteu mwanasiasa asiye na umaarufu Sarah Palin gavana wa Alaska kama mgombea mweza.

Wapiga kura walianza kutilia shaka hali yake ya kutokuwa na ujuzi na matokeo mabaya kwenye mijadala na televisheni hali iliyoyumbisha kampeni ya chama cha Republican.

Kwa kushindwa katika matumuzi, McCain alishindwa, na Obama akaingia Ikulu.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.