Na Jeshi la Polisi.
Jeshi la Polisi
nchini limewahakikishia wananchi kuendelea kuwepo kwa hali ya usalama na Amani
hapa nchini ikiwa ni pamoja na kuendelea kuwepo kwa hali ya utulivu na usalama katika
chaguzi ndogo.
Kauli hiyo imetolewa
na Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro mjini Moshi Mkoani Kilimanjaro
wakati akiwa katika ziara katika Shule ya Polisi Moshi (CCP) ambapo aliweza
kuzungumza na Wakufunzi na Askari waliopo mafunzoni Chuoni hapo ikiwa na lengo
la kukagua mwenendo wa mafunzo yanayoendelea katika Vyuo vya Polisi nchini.
IGP Sirro amesema katika
maeneo yaliyofanya uchaguzi mdogo hali ilikuwa shwari licha ya kuwepo kwa
matukio madogo ambayo yanaendelea kushungulikiwa na upelelezi utakapokamilika
majalada yao yatapelekwa kwa Waendesha mashtaka kwa hatua zaidi.
“ Hali iliuwa shwari
na ni wazi kuwa wananchi sasa wameelewa umuhimu wa kutii sheria bila ya kushurutishwa na natoa rai waendelee kudumisha
hali hiyo ikiwa ni pamoja na kutoa taarifa za Wahalifu na uhalifu katika maeneo
yao” Alisema Sirro.
Katika hatua nyingine akiwa Shule ya Polisi Moshi zamani CCP
IGP Sirro alitoa pongezi zake kwa Walimu
na Uongozi kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuwapika Askari hususani katika
mafunzo yao ya awali ambapo ametaka kila Askari kutambua wajibu wake.
Kwa upande wake Mkuu
wa Shule ya Polisi Moshi Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP)
Ramadhani Mungi amesema Chuo hicho kinaendelea kutoa mafunzo kwa umakini mkubwa
ili kuhakikisha kuwa kila Askari anayetoka anakuwa na ukakamavu wa kutosha na nidhamu
ya kuwahudumia Wananchi licha ya kuwepo kwa Changamoto za madeni ya maji na
umeme.
Alisema wanaendelea
kuboresha miundombinu ya Chuo hicho kwa kutumia miradi iliyopo ili kukiweka
katika hali ya usalama zaidi ikiwemo kujenga uzio imara kuzunguka maeneo hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.