ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 15, 2018

SAUTI:- RC OLE SENDEKA ATOA SIKU 15 MILIONI 41 KURUDISHWA.



GSENGOtV
Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Christopher Ole Sendeka, amewataka watumishi wa halmashauri ya wilaya ya Makete waliotumia vibaya fedha za miradi ya maendeleo wilayani humo zaidi ya milioni 41 zirudishwe kabla ya tarehe 30 mwezi huu.

Ole Sendeka, ametoa agizo hilo katika kikao cha madiwani wa halmashauri hiyo na kujadili hoja za mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambapo amewataka madiwani kusimamia na kuhoji fedha za miradi ya maendeleo ili kuwezesha fedha hizo kufanya kazi kama zilivyokusudiwa.

Katika mkutano huo kubwa lililoibuka ni upotevu wa miradi ya Afya katika halmashauri hiyo ziliztolewa kwa msaada wa shirika la kuhudumiwa watoto Duniani UNICEF, Shilingi milioni 41 ambapo baadhi ya wataalamu wamehusishwa na upotevu huo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.