ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 3, 2018

WAZIRI JAFFO AMMWAGIA SIFA RC MAKONDA KWA KUWAJALI WALIMU


 NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOTV


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo amemwaga Sifa kwa Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda kwa jitiada binafsi za kuwaboreshea Walimu mazingira ya kazi  ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za walimu.

Waziri Jaffo ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Pikipiki 2,894 zenye thamani ya zaidi ya shilling Billion 8.5 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kitaifa Zoezi hilo limefanyika Dar es salaam.

 RC Makonda amesema anajivunia kuona Dar es salaam inaendelea kushika kidedea kwenye matokeo ya mitihani ya kitafa kutokana na walimu kuwekewa mazingira bora ya kazi ikiwemo ujenzi wa ofisi 402 za kisasa za walimu, mikopo ya viwanja vya bei nafuu pamoja na kusafiri Bure kwenye daladala na Treni ambapo amesema bado ipo mipango mingi ya kuhakikisha walimu wake wanaishi vizuri ili wawe na motisha ya kazi.
 Aidha RC Makonda amesema pikipiki zilizotolewa zitaenda kuongeza nguvu na hari ya kazi kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kwa mkoa wa Dar es salaam umepata pikipiki kwa kila Kata.

 Pikipiki 2,894 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu Kata nchi nzima zimenunuliwa na wizara ya elimu na wafadhili kutoka Global Partnership in education kwa lengo la kuwawezesha kuzitembelea shule kwenye Kata zao ili kuboresha elimu.
Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam Mhe. Paul Makonda (kulia) akimkaribisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI Mhe. Suleiman Jaffo katika hafla ya uzinduzi wa Pikipiki 2,894 zenye thamani ya zaidi ya shilling Billion 8.5 zilizotolewa kwa waratibu wa elimu Kata ambapo kitaifa Zoezi hilo limefanyika Dar es salaam.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.