ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Katika kuimarisha miundombinu ya Elimu, Afya, mazingira na Michezo, Leo Mfuko wa Pesheni kwa Mashirika ya Umma NSSF umekabidhi mifuko 580 ya sariji kwa kituo cha Angelina Foundation ili kuwa sehemu ya usukumaji wa harakati za uboreshaji miundombinu Jimbo la Ilemela mkoani Mwanza.
Akikabidhi mifuko hiyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NSSF, Matson Mwakila ambaye ni Kaimu Meneja Kiongozi wa NSSF Mwanza amesema kuwa sera ya kurudisha fadhila kwa jamii kwa kusaidia miradi ya maendeleo imewasukuma kutimiza hilo sanjari na kuziona juhudi za wazi za Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Angelina Mabula, ambaye amekuwa akihangaika usiku na mchana kubuni njia na miradi mbalimbali ili kuwanusuru watu wa Jimbo lake na changamoto walizonazo.
Mfuko
wa hifadhi ya Jamii wa NSSF pamoja na Kampuni ya Mwanza Huduma wameamua
kumuunga mkono Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula kwa
kumkabidhi mifuko mia nane na themanini ya Saruji yenye thamani ya zaidi ya
shilingi milioni kumi na tano kwaajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo
Akizungumza
wakati wa makabidhiano hayo, Mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa mfuko wa hifadhi
ya jamii NSSF ndugu Matson Mwakila amesema kuwa NSSF ni mfuko wa jamii wenye
sera ya kurudisha fadhila kwa jamii inayowazunguka kwa kusaidia utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo kwa jamii ikiwemo miradi ya afya, elimu, michezo
na mengineyo yenye umuhimu mkubwa kwa jamii, Kupitia ombi
lililowasilishwa na taasisi yake ya mbunge wa jimbo la Ilemela ya The Angeline Foundation
kuamua kusaidia jamii hiyo
‘…
Sisi NSSF tutaendelea kuunga mkono serikali na viongozi wake katika kutekeleza
miradi mbalimbali ya maendeleo ili kumaliza kero na changamoto zinazoikabili
jamii, Pia niwaombe watu wengine kutushirikisha wakati wowote watakapohitaji
msaada wetu na mara zote tutaendelea kufanya hivyo …’ Alisema
Kwa
upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Mwanza Huduma ndugu Zully Nanji mbali na
kumhakikishia ushirikiano mbunge huyo amesema kuwa kitendo cha
kumuunga mkono mbunge huyo si mara ya kwanza na ataendelea kufanya hivyo ili
kumaliza kero na changamoto zinazoikabili jamii
Akihitimisha
makabidhiano hayo mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula
amewashukuru wadau hao kwa kumuunga mkono huku akiahidi kuitumia saruji hiyo
kwa kufyatulia tofali zitakazotumika kukamilisha maboma ya majengo ya madarasa,
zahanati au ofisi za taasisi za umma kulingana na mahitaji huku akiwaomba
wananchi na viongozi kuendelea kushirikiana.
Makabidhiano
hayo yalishuhudiwa na mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga,
Kaimu mkurugenzi Daniel Batare na viongozi wengine mbalimbali.
‘ Ilemela ni yetu, tushirikiane
kuijenga’
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.