ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 30, 2018

MUFTI MKUU TANZANIA AONGOZA MAELFU KATIKA MAZISHI YA SHEKHE MKUU WA MKOA WA MWANZA



GSENGOtV

Mufti Mkuu wa Tanzania Shekh, Abu Bakari Zuberi jana (Jumapili ya tarehe 29 July 2018) ameongoza mazishi ya aliyekuwa Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Sheikh Salum Fereji, aliyefariki dunia juzi usiku katika Hospital ya Bugando alipokuwa akipatiwa matibabu.


Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye mwenyeji wa ugeni mkubwa uliofurika toka maeneo mbalimbali Afrika Mashariki na kuweka himaya kwa muda mkoani pake kuhudhuria msiba huo mkubwa uliogusa mioyo ya wengi si waislamu pekee bali pia dini na madhehebu mbalimbali.

Marehemu aliwahi kuwa Mbunge wa jimbo la Geita Msalala wakati huo kati ya mwaka 1975-1980 na pia amekuwa muasisi wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambayo imekuwa suluhisho la migogoro mbalimbali Kanda ya Ziwa na Mfano wa kuigwa Tanzania Bara.


Innalillahiwainnailaihirojiun

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.