Katibu
Mkuu Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Dkt. Bashiru Ally ametembelea maonesho ya
42 ya Biashara ya Kimataifa almaarufu Sabasaba yaliyopo katika viwanja vya
Mwalimu Nyerere wilayani Temeke ili kujionea utekelezaji wa ilani ya uchaguzi
ulivyo kwenye maonesho hayo.
Dkt.
Bashiru Ally alipokelewa na Naibu Waziri Viwanda, Biashara na Uwekezaji Enjinia
Stellah Manyanya na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara
Tanzania (TanTrade) Ndugu Edwin Rutageruka ambaye alizungushwa kwenye mabanda
mbalimbali ya viwanjani hapo yakiwemo banda la NSSF, Banda la Mamlaka ya mapato
Tanzania (TRA), banda la Chuo kikuu, banda la Bunge, banda la JKT, banda la
Maliasili na utalii, banda la TBC, banda la Takukuru, Banda la Umoja wa
wafanyabiashara wanawake Tanzania, banda la Watu wa Zanzibar pamoja na banda la
kampuni ya simu la TTCL.
Katika
majumuisho mara baada ya kutembelea maonesho hayo, Dkt. Bashiru Ally amesifu
maonesho ya mwaka huu yamejaza Wafanyabiashara Wazalendo wengi, pia
amefurahishwa na fursa mbalimbali za kiuchumi na ajira hali iliyompelekea
kutamani maonesho hayo yafanyike na upande wa Zanzibar pia.
“Utekelezaji
wa ilani ya uchaguzi umejionyesha dhahiri kwenye maonesho haya. Natamani na
Watu wa Zanzibar nao pia wapate fursa ya kuwa na maonesho kama haya ili nao
waweze kuona, kujifunza na kutanua wigo wa ajira na biashara. Natoa rai suala
hili mlipokee na mlifanyie kazi pia” alisema Dkt. Bashiru Ally.
Pia
Dkt. Bashiru amesifu utaratibu uliowekwa wa kuwa na matukio mbalimbali kila
siku kwenye maonesho hayo. Matukio hayo ni kuwa na siku ya mazingira, rushwa, asali, sanaa na utamaduni ambayo
yalishirikisha jumla ya Watu 2560.
“Malengo
ya ilani ya uchaguzi yamejikita kwenye uchumi, ajira, rushwa na ufisadi pamoja
na amani na usalama. Nawapongeza kwa kuwa na siku ya rushwa. Hongereni kwa
kujumuika nasi kwenye kupambana na rushwa na kutangaza mafanikio ya mapambano
hayo ya rushwa yanayofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Dkt. John
Magufuli.
Katika
msafara wake Katibu Mkuu wa CCM, Dkt. Bashiru Ally aliambatana na Naibu Katibu
Mkuu CCM, Ndugu Rodrick Mpogolo, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa,
Kanali Mstaafu Ngemela Lubinga, Katibu Mkuu Jumuiya ya Wazazi Ndugu Erasto
Sima, Katibu Mkuu Jumuiya ya Wanawake (UWT) Queen Mlozi, Katibu Mkuu Jumuiya ya
Vijana (UVCCM) Mwl. Raymond Mwangwala pamoja na maofisa mbalimbali toka CCM
Makao Makuu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.