NA ZEPHANIA MANDIA/GSENGOtV
Halmashauri za wilaya na miji nchini zimetakiwa kutenga fedha kwa ajili ya kuwaendeleza walimu wa michezo ili kukuza na kuendeleza sekta ya michezo katika shule za msingi na sekondari.
Agizo hilo limetolewa na mkurugenzi wa sera na mipango katika wizara ya habari, sanaa, utamaduni na michezo PETRO LYATUU wakati wa mahafali ya saba ya chuo cha maendeleo ya michezo cha MALYA wilayani kwimba mkoani mwanza.
Naye mkuu wa chuo hicho RICHARD MGANGA amesema chuo hicho kinakabiliwa na changamoto lukuki zinazozorotesha jitihada za kuwaanda wataalam wa michezo ikiwemo uhaba wa mabweni pamoja na vifaa vya michezo.
Jumla ya wahitimu zaidi ya 40 wametunukiwa astashahada na stashada katika fani mbalimbali za michezo wakati wa mahafali hayo, MWANAHAMISI MWIYOMBO ni mmoja wa wahitimu hao
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.