ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 9, 2018

YALIYOJIRI JIJINI MWANZA WAKATI WAZIRI MKUU AKIHITIMISHA MAADHIMISHO YA SIKU YA USHIRIKA DUNIANI. Mhe John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza apata Tuzo kwa juhudi zake katika kurejesha mali za Chama Kikuu cha Ushirika cha Nyanza (NCU), tuzo hiyo imetolewa na wana ushirika ambapo Mhe Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) aliikabidhi katika kilele cha siku ya ushirika Dunia, iliyoadhimishwa kitaifa Jijini Mwanza.
Tuzo hiyo ya Mhe John Mongella, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ilipokelewa na Mhe Zainabu Telack Mkuu Wa Mkoa wa Shinyanga na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa niaba yake. Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza alitumia fursa hiyo kuishukuru Serikali ya awamu ya Tano chini ya uongozi wa Mhe. Dkt John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika juhudi zake za kuendeleza sekta ya ushirika. Pia, Mhe. Zainabu Telack Mkuu Wa Mkoa wa Shinyanga na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Mwanza alimshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoendelea kuifanya kwa kufufua na kuendeleza Ushirika Nchini kwani Mhe Waziri Mkuu amekua na mchango mkubwa katika urejeshwaji wa mali za Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU) ambazo zilikua zimeporwa na watu wachache kwa maslai yao binafsi. Katika zoezi hilo la urejeshwaji wa mali za Chama Kikuu cha Ushirika Nyanza (NCU), mali saba kati ya kumi zimerejeshwa na utaratibu unaendelea mali tatu zilizo salia ziweze kurejeshwa. Pia Mhe Waziri Mkuu aliwapongeza wana Mwanza kwa kupokea na kuridhia sherehe za siku ya ushirika Duniani kitaifa kufanyika Jijini Mwanza. Mhe Waziri Mkuu alieleza ilani ya Chama cha CCM ya 2015 inaelekeza kuimarisha na kuviendeleza vyama vya ushirika kwa kuwa , Ushirika ni fursa na una tija kubwa kwa wakulima kwa maendeleo ya Taifa letu kufikia Uchumi wa kati. Kauli mbiu ya siku ya ushirika Dunia kwa Mwaka 2018 ni “Ushirika kwa ulaji na uzalishaji wa bidhaa na huduma”

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.