A..kibao cha bandari ya nyamirembe. |
Fursa Nyingine Geita;Bandari ya Nyamirembe kufufuliwa
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi
na Mawasiliano, Mhe. Mhandisi Isack
Aloyce Kamwelwe (MB), ametembelea na kuona miradi mbalimbali inayotekelezwa
Mkoani Geita akiambatana na Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, Mkuu wa Wilaya ya Chato Mhe. Shaaban Ntarambe, Mkurugenzi wa
Mamlaka ya Bandari Mhandisi Deusdedith
Kakoko, pamoja na Meneja wa TANROADS Mkoa wa Geita Mhandisi Harun Senkuku.
F.waziri wa ujenzi, uchukuzi na mawasiliano, mhe. eng. isack aloyce kamwelwe (kulia) akipeana mkono wa kwaheri na mkuu wa mkoa wa geita mhe.eng robert gabriel |
Miradi aliyoitembelea ni
pamoja na Bandari ya Nyamirembe iliyoko kijiji na Kata ya Nyamirembe Wilayani
Chato ambayo ilikua ikitumika tangu enzi ya Mkoloni ambayo kwa sasa haifanyi
kazi. Mhe. Waziri amewaeleza wananchi wajiandae kufurahi kwani muda si mrefu
bandari hiyo itafufuliwa na kuanza kazi; ni baada ya kujitokeza kumlaki kwa
fuaraha baada ya kumuona akitembea kwenye bandari hiyo.
E.barabara ya bwanga-biharamulo |
Amesema “mwezi wa nane mwaka huu tunasaini mkataba,
tunairudisha Bandari ya Nyamirembe. Na sasa tunajenga meli kubwa, itakayokuwa
na uwezo wa kubeba abiria elfu moja mia mbili (1,200), mizigo tani mia nne
(400) ambayo itapita hapa kwenda Bukoba ndiyo maana kituo hiki lazima tukijenge
na mkandarasi anaingia hapa mwezi wa nane. Hivyo ni ushindwe mwenyewe mwananchi
kwa sababu sasa meli itakuwepo, barabara ya lami ipo, kiwanja cha ndege kinaendelea
kujengwa unataka nini tena?” alimaliza kwa kushangiliwa na wananchi.
Kisha, Mhe. Waziri amembelea
na kujionea maendeleo ya hatua ya ujenzi wa barabara ya Bwanga – Biharamulo
yenye urefu wa kilomita sitini na saba (Km.67) inayojengwa kwa kiwango cha lami
na kufurahishwa na hatua iliyofikiwa baada ya kupewa taarifa kuwa, barabara
hiyo imeshajengwa hadi kilomita hamsini na saba (Km.57) hivyo bado kilometa
kumi (Km.10) ili iweze kukamilika.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Mhandisi Gabriel amemshukuru Mhe.
Waziri kwa ujio wake lakini pia kwa kuteuliwa kuwa msimamizi wa wizara hiyo na kupendekeza maombi ya kutanuliwa
barabara za kuingia Geita mjini ili ziwe mbili wakati wa kuingia na mbili wakati
wa kutoka, lengo ikiwa ni kupunguza ajali na kuokoa maisha ya watumia barabara
waendesha baiskeli na watembea kwa miguu ambao hupata ajali kutokana na
msongamano barabarani.
Mkuu wa Mkoa pia ametumia nafasi hiyo kuomba Daraja la Wavuka
kwa Miguu (Pedestrian Bridge) karibu na soko jipya la kisasa Mjini Geita
litakalokuwa na duka lenye bidhaa zinazotengenezwa Tanzania pekee katika
kutafuta soko la bidhaa za ndani, jambo lililopelekea Mhe. Waziri kusema
amelipokea ombi hilo na kuahidi kulishughulikia kwa kumuagiza Meneja TANROADS
Mkoa kuandaa maombi hayo na kumwasilishia ili aweze kusaidia utekelezaji wake.
B.. mkuu wa mkoa wa geita, mhe.eng robert gabriel akiwa(mweye kofia nyeusi-kulia) , mkurugenzi wa mamlaka ya bandari,eng deusdedith kakoko, (kushoto) wakitembea bandarini |
C.waziri wa ujenzi,uchukuzi na mawasiliano, eng. isack aloyce kamwelwe (koti la mistari, wapili mbele kushoto) na alioambatana nao wakitafakari jambo. |
Kisha alimshukuru Mhe. Waziri kwaniaba ya wananchi wa Geita kuendelea kufungua
milango ya fursa na kutoa wito kuhusiana na jukwaa la fursa za biashara
litakalofanyika mkoani Geita kuanzia tarehe 15 hadi 16.08.2018 na kwamba endapo
bandari hiyo itakamilika, uwanja wa ndege ukakamilika, basi wageni wengi
watakuja kwani kuna vivutio vya utalii lakini pia biashara ya dhahabu.
Kwa upande wake Mkuu wa
Wilaya ya Chato, Mhe. Shaaban Ntarambe
alimhakikishia Mhe. Waziri kuwa, wananchi wapo tayari kupokea maendeleo na
ameshukuru kwa namna ambavyo mkandarasi anayejenga barabara hiyo ana mahusiano
mazuri na wananchi wa Chato jambo linalosaidia utekelezaji mzuri wa mradi usiwe
na migogoro.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.