ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 11, 2018

HATUA KALI KUCHUKULIWA DHIDI YA WATAKAO WAOZESHA WANAFUNZI KWA NIA YA KUJPATIA MAHARI.GSENGOtV
Serikali wilayani  MISUNGWI mkoani MWANZA  imekemea tabia ya baadhi ya wazazi na walezi kuwalazimisha watoto wao wa kike kufeli mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi ili wawaozeshe kwa nia ya kupata mahari.

Mkuu wa wilaya hiyo JUMA SWEDA (wa pili kutoka kulia aliyeketi) amesema hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wazazi na walezi watakaob ainika kuwaozesha wanafunzi kwa nia ya kupata mahari pamoja na wale wanaokatisha ndoto zao za kitaaluma kwa kuwapa ujauzito. Aliyesimama na kipaza sauti ni Mkurugenzi wa Wilaya ya Misungwi Eliurd Mwaiteleke akitoa somo.
Yasin Ally.

Mkurugenzi mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na wasichana la KIVULINI YASINI ALLY akibainisha sababu zinazo kwamisha watoto kuendelea na masomo katika uzinduzi wa kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia kwenye kata ya mabuki wilayani MISUNGWI.
Tabia hiyo inayokwamisha watoto wa kike kutimiza ndoto zao za kitaalamu imekemewa vikali na familia mbalimbali zilizokusanyika hapa.

Kampeni ya kutokomeza ukatili wa kijinsia inatekelezwa na halmashauri ya wilaya MISUNGWI kwa kushirikiana na shirika la KIVULINI kufuatia kushamiri kwa tabia ya baadhi ya wanaume kutumia fedha za mauzo ya mazao kwa matumizi ya anasa.

Kampeni hiyo itakayodumu kwa muda wa miezi miwili itaendeshwa katika vijiji vyote 113 vya wilaya misungwi ili kufikisha elimu kuhusu madhara ya ukatili wa kijinsia kwenye jamii.


 Akinamama wamefunguka juu ya yale yanaowazunguka.
Burudani ngoma asili.
Jamii imeamua na sasa kilichobaki ni utekelezaji.
Raha ndani ya kusanyiko.
Michezo mingine waachie wenyewe.
Utalii ndani ya kusanyiko la elimu darasa.
Kwaya ya wanafunzi ikielimisha kwa njia ya uimbaji.
Jambo la msisitizo.
Eneo la kusanyiko.
Ukimya wananchi wakifuatilia yanayojiri.
Mwamko umekuwa ni mkubwa kwa wananchi hii ikidhihirisha kuwa kile kinacho jadiliwa hapa kimewagusa kiasi gani.
Kaya kwa kaya ndani ya kusanyiko.
Jiografia ya eneo la tukio.

KAZI DARASA

Yafuatayo ni mambo yatakayosaidia kumuongoza binti yako kuepuka kujiingiza katika ngono akiwa na umri mdogo.

Mwambie mwanao wa kike kuwa unampenda na mkumbatie kwa upendo mara kwa mara. Inashauriwa jambo hili alifanye mzazi wa kiume mara nyingi ili mtoto azoee kulipokea kutoka kwa jinsia ya kiume. Mtoto pia hatozuzuliwa na mapenzi toka kwa mwanaume baki.

Mwambie mwanao ni mrembo kila mara, wazazi wote wanashauriwa kuzungumza na mtoto wao wa kike na kumsifia juu ya urembo wake lakini baba akitekeleza jukumu hili inakuwa inamjenga zaidi mtoto juu ya kujitambua na kutosumbuliwa aambiwapo hivyo na mwanaume anaemtaka kingono. Mfundishe jinsi ya kujibu aambiwapo hivyo, msifie kwa kumwambia ana macho mazuri, umbo zuri, mpe sifa zote wazitumiazo wanaume kuwarubuni watoto wa kike.

Mfunze mwanao kuridhika na hali halisi ya uchumi wa familia. Fanya mazungumzo na mwanao wa kike juu ya hali halisi ya maisha hapo nyumbani ili umuweke bayana juu ya kipato cha familia. Mnapataje fedha? Mnazitumia katika vipaumbele vipi? Mwandae kuridhika na anachopewa nyumbani na kuepuka ‘hongo’ ndogondogo kwani tafiti zimeonyesha vijizawadi kama pipi, mafuta ya kupakaa na manukato, soda na hata miwa hutumiwa na wanaume kuwarubuni mabinti hasa wanapokuwa shuleni.

Wazazi (hasa mama), mueleze bayana mtoto wa kike kuwa madhara mengi yatokanayo na tendo la ngono ni mzigo kwake kubeba. Atambue kuwa kubeba mimba ni rehani hasa katika umri mdogo. Kwamba kuna kufa au kupona katika miezi tisa ya ujauzito hasa kwa watoto. Kwamba yapo magonjwa ambata ya kila aina. Atambue namna ilivyo aibu kwa familia na unyanyapaa atakaoupata kuanzia ngazi anapotoka hadi aingiapo. Pia mueleze bayana kuwa ngono na mimba hazitouacha mwili wake salama kimwili, kiakili na kama anamwamini Mungu – kiimani anakuwa katenda dhambi.

Elimu ya afya ya uzazi isiachwe nyuma. Wazazi tuache dhana ya kwamba kuongea na mtoto masuala ya uzazi ni aibu. Zungumza juu ya mabadiliko ya kimwili na maumbile. Mbona chuchu zinatokea? Ajue mimba inapatikana kwa kujamiiana – athari za ngono kama gonjwa na ukimwi na mambo mengine namna hii. Mueleze jinsi ya kuepuka ‘mihemko’ ya kibaolojia inayomsukuma kuwaza ngono. Kwamba anaweza kutumia muda huo kufanya mazoezi au kulima bustani ya mboga, nk. na kujishughulisha na mambo ya msingi kwa maendeleo yake.

Mfunze mwanao kutokuamini mtu yeyote wa jinsia ya kiume. Mapema binti yako ajue linapokuja suala la ngono – ndugu wa karibu katika familia tandaa na rafiki wa familia wako mstari wa mbele kama ‘waharibifu’. Jenga mawasiliano na mahusiano ya karibu na binti yako ili upate fursa ya ‘kuhadithiwa’ njama za ‘wanaomnyemelea kingono. Kama hakuna ‘ukaribu’, mjengee. Vipi akushirikishe katika changamoto anazokutana nazo za vishawishi vya kingono?

Watoto wa kiume wasiachwe nyuma. Wafundishe wavulana kuthamini utu na maisha ya dada zao na watoto wenzao wa kike kwa ujumla. Wafunze kuuthamini mchango wa mama zao katika maisha yao na jamii kwa ujumla. Wazazi wa kiume tuwe taswira kwa watoto wetu wa kiume kwa kuwaheshimu mama, dada, shangazi na watoto wetu wa kike kwa kuwapatia mapenzi na fursa sawa ndani ya familia. Akina baba tuache ngono na watoto wakike huku tukibainisha namna gani tungependa kuwalinda na kuwasaidia kuzifikia ndoto zao pale tunapozungumza na watoto wa kiume.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.