ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 11, 2018

UFARANSA HAOOoooo FAINALI KOMBE LA DUNIA 2018

Mabingwa wa Dunia 1998 Ufaransa wametinga fainali ya Kombe la Dunia baada ya kungoja tangu 2006, kwa kuilaza Ubelgiji 1-0 St. Petersburg.
Mbali na kuwaondoa red devils wa Ubelgiji kutoka Kombe hili, Ufaransa Imevunja rekodi ya kutofungwa kwa vijana wa Martinez walioepuka kichapo mechi 24 kabla ya leo.
Kylian Mbappe, staa wa Ufaransa, ambaye hakuzaliwa wakati timu hii iliinua taji la Kombe la Dunia 1998, ni mmoja wa wachezaji waliochangia pakubwa ushindi huo.
Vijana wa Didier Deschamps waliendeleza fomu yao nzuri Urusi kwa kuizima timu ya Ubelgiji iliyopachikwa 'Kizazi cha dhahabu'kupitia bao la mlinzi Samuel Umtiti kunako dakika ya 51.
Nahodha wa Ubelgiji Hazard, ambaye kabla ya mechi hii alifunga mabao mawili na kuchangia ufungaji wa mengine mawili Kombe la Dunia, alizingirwa na wachezaji wa Ufaransa waliosalia naye ana kwa ana kila alipopokea pasi.
N'golo Kante na Paul Pogba walijenga ukuta mbele ya ngome yao na kulinda bao lao hadi kipenga cha mwisho.
Kufikia sasa Ufaransa imefungwa tu mabao manne ikiwemo matatu dhidi ya Argentina na moja dhidi ya Australia.
Licha ya kipute hicho kutoka sare kipindi cha kwanza, mabao yangekuwa mengi ila tu ustadi wa wadakaji Courtois na Lloris haukurusu mkwaju kutua wavuni.
Mbinu za mkufunzi Martinez hazikufaulu safari hii licha ya kufanya mabadiliko ya kusaka mabao.
 Cristiano Ronaldo atua Juventus
Wilshere ajiunga na West Ham,
 Torreira 'aelekea' Arsenal
Kiungo Mertens na mfungaji Batshuayi hawakuwatatiza mabeki wa Ufaransa wakiongozwa na Varane na Umtiti. Ingawa Mertens alionekana kubadili huduma kutoka wingi ya kulia kwa krosi zake safi, Lukaku hakufanikiwa kuzigeuza kuwa magoli.
Wakati huo huo, kurudi kwa kiungo mkabaji wa Ufaransa Blaise Matuidi, iliipiga jeki timu hiyo.
Matuidi aliboresha ushirikiano kati ya mabeki na washambuliaji wa Ufaransa.
Hata hivyo, Ubelgiji itacheza Jumamosi tarehe 14 Julai kuwania nafasi ya tatu ugani Krestovsky.
Ni mara ya tatu Ufaransa kutua fainali na mafaniko hayo yamekuwa ni nafuu kwani ilikuwa ni jaribio lao la saba.
Kwa upande mwingine itakuwa ni uchungu Ubelgiji iliyokuwa ikisaka bahati kwa mara ya pil tangu Argentina kukatiza ndoto zake mnamo 1986.
Kwa sasa meneja wa Ufaransa Didier Deschamps huenda akaweka historia kwa kuwa mshindi wa Kombe la Dunia akiwa mchezaji na mkufunzi kama vile Mario Zagallo na Franz Beckenbauer Iwapo ataisaidia Ufaransa kuondoka na Kombe la Dunia Jumapili ijayo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.