Mhe. Seleman Jafo, akizungumza wakati wa Hafla ya kuwapatia Vitambulisho Wazee wa Jiji la Dodoma.
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma akitoa salam za jiji muda mfupi kabla ya zoezi la ugawaji wa Vitambulisho kwa wazee halifanyika.
Mmoja ya Wazee akipokea kitambulisho mara baada yakuzinduliwa kwa zoezi lakuwapatia vitambulisho wazee Jiji la Dodoma.
Picha ya pamoja kati ya Mhe. Waziri Viongozi wa Halmashauri na wazee waliopatiwa vitambulisho.
Mhe. Diwani wa Kata ya Mkonze akishukuru kwaniaba ya wananchi wa Mkonze.
Makatibu Tawala wa Mikoa Waagizwa
Takwimu za Wazee ifikapo 30 Juni, 2018
Na. Atley Kuni-OR TAMISEMI
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb), amewaagiza
Makatibu Tawala wa Mikoa Tanzania Bara kuwasilisha taarifa za takwimu za wazee
ifikapo 30, Juni 2018.
Waziri Jafo, alitoa kauli
hiyo mapema leo alipokuwa akizindua
zoezi la kuwapatia vitambulisho maalum
wazee wapatao 1,118 wa Jiji la Dodoma kutoka kata za Mkonze, Mnadani, Uhuru,
Madukani, Makole na Majengo. Vitambulisho hivyo, pamoja na mambo mengine
vitawawezesha wazee hao kupata huduma za afya bure na kwa wakati.
“Ifikapo tarehe 15 Juni,
2018 kila kata iwe imetambua wazee na ifikapo tarehe 22 Juni, 2018 kila
Halmashauri iwe imeunganisha taarifa za wazee kutoka katika kata zake zote”
alisema Waziri. Aidha Waziri Jafo aliagiza kuwa, “ifikapo Juni, 26, 2018 kila
Mkoa uwe umeunganisha taarifa zote na kuzituma kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais
TAMISEMI”.
Aliwaonyawale wote watakaoshindwa kutimiza agizo hilo kuchukuliwa
hatua kulingana na miongozo, kwasababu watakuwa wameshindwa kutekeleza wajibu
wao.
Kwa upande wake Mkurugenzi
wa Jiji la Dodoma Ndugu Godwin Kunambi akizungumza katika hafla
hiyo alisema shabaha ni kuwafikia wazee wote kwenye Jiji hilo, na kubainisha
kwamba, vitambulisho wanavyo vitoa kwa wazee hao vitatumika pia kuwapa
kipaumbele wazee sehemu zote za kutolea huduma hususan ofisi za serikali.
“Mhe. Waziri tunataka
vitambulisho hivi tunavyo wapatia wazee wetu leo viwasaidie pia kupata huduma
kwa haraka na kwa wakati pindi wanapofika kwenye ofisi zingine za Serikali”
alisema Kunambi.
Mbali na kutolea ufafanuzi
wa matumizi ya vitambulisho hivyo, Mkurugenzi Kunambi alisema juu ya Jiji hilo
lilivyo jipanga katika suala zima la makusanyo ya mapato ya ndani, ambayo ndio yamekuwa
chachu ya kuboresha huduma za afya kwa makundi maalum hususan wazee.
“Mhe. Waziri, Jiji
limepanga kukusanya Bil. 68 katika mwaka wa fedha ujao ikilinganishwa na mwaka huu
wa fedha ambapo tulijiwekea lengo la kukusanya Bil. 20 nahadi kufikia mwezi
Februari tulikuwa tumekusanya Bil. 14”. Kunambi ameongeza kuwa, katika mwaka
ujao wa fedha wametenga kiasi cha Mil. 58 kwaajili yakuwezesha huduma za wazee
kwenye Jiji hilo.
Naye Kaimu Mkuu wa Wilaya
ya Dodoma Mjini ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Kongwa Mhe. Deo Ndejembi,
ametumia fursa hiyo kuwaonya baadhi ya watendaji wanao waambia wazee kwamba
hakuna dawa.
“Kumekuwepo na malalamiko
mengi siku za nyuma kutoka kwa wazee kuwa, baadhi ya watendaji wa afya wanawanyanyapaa
wazee na kuwaambia hakuna dawa wafikapo vituoni, sasa Mhe Waziri, mimi niliseme
kwa uwazi kabisa hatuta mvumilia mtu yeyote atakaye onekana ni kikwazo kwa
wazee hawa kadi zimetoka wazee wahudumiwe, sio mnajiwekea vijiduka karibu na
vituo halafu mnawaambia waende waka nunue” alionya Ndejembi
Awali akitoa taarifa ya
uandaji wa vitambulisho Mganga Mkuu wa Jiji la Dodoma, Dkt. Mohamed Nyembea,
alisema utekelezaji wa zoezi hilo ulianza kwa hatua za awali kwa kuwatambua
wazee katika Kata 41 za Jiji la Dodoma, ambapo jumla ya wazee 15,885 kutoka
kata 33 miongoni mwa 41 wamekwisha tambuliwa
na miongoni mwao wanawake ni 9,132 na wanaume ni 6,753 ambapo ni sawa na
asilimia 80.5 ya kata zote 41 za Jiji la
hilo.
Utoaji wa vitambulisho kwa
wazee ni utekelezaji wa sera ya Taifa ya wazee ya mwaka 2003 ambapo
inazungumzia mambo muhimu ya wazee ikiwepo kutenga dirisha maalum katika vituo
vya kutolea huduma za afya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.