GSENGOtV
Changamoto ya rasilimali fedha kwa baadhi ya vituo vya huduma za afya nchini imekuwa kikwazo katika uboreshaji wa huduma hizo kiasi cha kuifanya sekta hiyo kutofikia malengo yanayotarajiwa.
Kwa kuliona hilo Benki ya CRDB nchini hii leo Tarehe 25 Mei 2018 imekabidhi hundi ya shilingi milioni 240, kwa ajili ya upanuzi wa idara ya wagonjwa mahututi ya hospitali ya rufaa ya Bugando (BMC) Jijini Mwanza, ili kukabiliana na tatizo la msongamano wa wagonjwa unaoikabili Hospitali hiyo.
Mkurugenzi mkuu wa Hospitali ya rufaa ya Bugando Dk. Abel Makubi, ameiomba serikali kutangaza ajira mpya za madaktari, ili kupunguza uhaba wa madaktari bingwa katika idara hiyo.
Akizungumzia matumizi ya fedha hizo kwa niaba ya mkurugenzi mtendaji wa Benki ya CRDB nchini Dk. Charles Kimei, kaimu mkurugenzi wa benki hiyo Esther Kileo, amesema msaada huo umetolewa, ili kurahisisha utoaji wa huduma kwa wagonjwa.
Kutokana na umuhimu wa upanuzi wa Idara hiyo, Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza Jude Thadeus Ruwaich, ambaye pia ni mwenyekiti wa bodi ya Hospitali hiyo, amesema msaada huo unahitajika, ili kutatua msongamano unaoikabili Hospitali hiyo.
Kaimu mkurugenzi wa benki ya CRDB Esther Kileo akimpa mkono Askofu mkuu wa Kanisa Katoliki Jimbo kuu la Mwanza Jude Thadeus Ruwaich mara wakati wa upigaji picha ya pamoja ya makabidhiano.
CRDB katika picha ya pamoja na viongozi.
Picha ya pamoja na wadau kitengo cha dharula.
Baada ya makabidhiano hayo katika hatua nyingine, Benki hiyo imelikabidhi Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza Pikipiki tatu aina ya Boxer, zenye thamani ya shilingi milioni kumi ikiwa ni pamoja na gharama za usajili, ili kuboresha shughuli za ulinzi na usalama kwa mkoa wa Mwanza.
Maelezo toka kwa mwenyeji kwa wageni.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Mwanza Ahmed Msangi akiwasilisha salamu za shukurani toka kwa IGP Simon Sirro kwa Kaimu mkurugenzi Benki ya CRDB nchini baada ya kupokea pikipiki 3 kama sehemu ya kuliwezesha jeshi hili kuhudumia wananchi.
Karibuni wageni.
Picha ya pamoja.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.