Waliofutwa uanachama ni pamoja na aliyekua Naibu Katibu Mkuu Bara, Getrude Ndibalema na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Kilimanjaro, Dickson Kibona.
Akizungumza leo Mei 22, katika mkutano na waandishi wa habari jijini Arusha, Ole Sosopi amesema kwamba uamuzi huo umekuja baada ya kufuata taratibu zote za kuwahoji kupitia tume iliyoundwa.
Amesema viongozi hao wamehojiwa baada ya kuwepo tuhuma za usaliti ambazo ni kosa kwenye chama hicho, Sosopi amesema Bavicha imeridhia kuwaondoa wanachama hao baada ya kujiridhisha kwa makosa waliyoyafanya.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.