ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 23, 2018

SAFARI YA MWISHO YA MASOGANGE KUKAMILIKA LEO MKOANI MBEYA.

MWILI wa msanii, Agness Gerald ‘Masogange’ tayari umeshawasili Nyumbani katika kijiji cha Utengule, Mablizi, mkoani Mbeya tayari kwa taratibu za mazishi.

Masogange alifariki dunia Ijumaa iliyopita katika kituo cha Huduma za Afya cha Mama Ngoma kilichopo Mwenge jijini Dar ambapo jana aliagwa katika Viwanja vya Leaders na kusafirishwa kwenda kwao kuzikwa.


SABABU ZA KIFO CHAKE.
Kwa mujibu wa Taarifa za awali wakati wa kuthibitisha juu ya kifo chake Agness mwanasheria wake, Reuben Simwanza alitamka kuwa taarifa za kifo chake amezipata kupitia dada yake, saa chache mara baada ya kupoteza uhai.

Kwa maelezo ya Simwanza, dada wa Masogange, Emma Gerald, ndiye aliyetoa taarifa hizo baada tu ya kutoka kumuona alipokuwa amelazwa katika Hospitali ya Mama Ngoma, Mwenge jijini Dar es Salaam.

Mwanasheria huyo ambaye amedai yeye si msemaji zaidi, kuhusu nini chanzo cha kifo chake, alidai mara ya mwisho waliwasiliana naye siku mbili zilizopita kwa ujumbe wa simu ya mkononi.

  “Unajua kuumwa kweli alikuwa anaumwa, kipindi cha kesi yake magonjwa ya hapa na pale ikiwamo presha, si unajua tena mambo ya kesi hayana mwenyewe, lakini baada ya kwisha tulikuwa tunataniana kwamba sasa nina imani utakuwa powa kwani kila kitu kipo sawa,”amesema Simwanza.

Hivi karibuni, Masogange alihukumiwa kulipa faini ya Sh 1.5 milioni  na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya kukutwa na hatia ya kutumia dawa za kulevya aina ya heroin.

Alibainika kutumia dawa hizo kati ya Februari 7 na 14, 2017

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.