Mchezaji hatari wa klabu ya soka ya Liverpool, Mohamed Salah ameshinda tuzo ya mchezaji bora wa mwaka inayotolewa na Chama cha Wachezaji wa kulipwa nchini England (PFA).
Salah ameshinda tuzo hiyo kwa kuwabwaga wachezaji wengine akiwemo Harry Kane (Tottenham Hotspur), David De Gea (Manchester United), Kevin De Bruyne, David Silva na Leroy Sane (Manchester City).
Wakati huo huo Leroy Sane ameshinda tuzo ya mchezaji bora chipukizi wa soka nchini Uingereza. Sane amewashinda Sterling (Manchester City), Ryan Sessegnon (Fulham), Harry Kane (Tottenham Hotspur) na Marcus Rashford (Manchester United).
Kwa upande wa soka la wanawake, Fran Kirby (24) wa klabu ya Chelsea amefanikiwa kushinda tuzo ya mchezaji bora wa wanawake ya PFA.
Naye Lauren Hemp wa Bristol City na timu ya wanawake chini ya umri wa miaka 19, amshinda tuzo ya mchezaji chipukizi kwa upande wa wanawake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.