ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 30, 2018

RAIS WA NIGERIA KUWA KIONGOZI WA KWANZA WA AFRIKA KULAKIWA NA DONARD TRUMP MAREKANI.



Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa la kutoka bara Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump White House atakapokutana na kiongozi huo kwa mashauriano rasmi mjini Washington baadaye leo.

Marais wengine wa Afrika wamewahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, wakiwemo Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya, lakini nje ya Marekani.

Rais Kenyatta alikutana na Trump pambizoni mwa mkutano wa G7 nchini Italia mwezi Mei mwaka jana, naye Rais Kagame akakutana na kiongozi huyo wa Marekani Januari mwaka huu mjini Davos, Uswizi pambizoni mwa mkutano mkuu kuhusu uchumi wa dunia.

Septemba mwaka jana, Rais wa Uganda Yoweri Museveni pia alikutana na kupigwa picha na Rais Trump kwenye dhifa iliyoandaliwa wakati wa mkutano wa viongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa jijini New York. Hakukuwa na mazungumzo yoyote hata hivyo na haikuwa ziara ya kikazi kwa Bw Museveni.

Wawili hao wanatarajiwa kujadiliana kuhusu masuala ya kiuchumi na kiusalama watakapokutana leo.

Lakini wengi watafuatilia kwa karibu mazungumzo hayo hasa baada ya Bw Trump kushutumiwa vikali kutokana na kuyaeleza mataifa ya Afrika kama ''machafu" au ya "mabwege" mapema mwaka huu.

Bw Trump alijitetea na kusema kwamba hakuwa anayabagua mataifa ya Afrika.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.