ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 29, 2018

RAIS KAGAME: MAHAKAMA YA ICC HAINA UADILIFU: IMEKUWA IKIWAANDAMA VIONGOZI WA AFRIKA TU.

Rais Kagame: Mahakama ya ICC haina uadilifu; imekuwa ikiwaandama viongozi wa Afrika tu
Rais Paul Kagame wa Rwanda kwa mara nyingine tena ameikosoa vikali Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC yenye makao yake The Hague Uholanzi na kusisitiza kwamba, imefeli katika kutekeleza uadilifu.

Rais Kagame amebainisha kwamba, Mahakama ya Kimataifa ya ICC imefeli katika utendaji wake kutokana na kushindwa kutekeleza uadilifu kwa wote na badala yake imekuwa ikialiandama tu bara la Afrika.
Rais wa Rwanda ameongeza kuwa, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilipaswa kutekeleza uadilifu kkatika pembe zote za dunia na sio kujihusisha tu na bara la Afrika.

Fatou Bensouda, Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC
Rais Kagame aidha amesema kwamba: "Mwanzoni mwa kuanzishwa mahakama ya ICC, nilisema kwamba, kulikuwa na msingi wa udanganyifu ambao ulianzishwa na jinsi utakavyotumiwa.
Niliwaambia watu kuwa hii itakuwa mahakamani ya kuwapandisha kizimbani Waafrika na sio watu kutoka katika kila pembe ya dunia. Sidhani kama nilikosea kusema hivyo."
Hayo yanajiri katika hali ambayo, viongozi wengi wa nchi za Zfrika wamekuwa wakikosoa vikali utendaji wa Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC, ambapo Rais Yoweri Museveni wa Uganda ni miongoni mwa viongozi wa Kiafrika wanaokosoa utendaji wa mahakama hiyo.
Itakumbukwa kuwa, mwezi Oktoba mwaka jana, Burundi ilikuwa nchi ya kwanza kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) baada ya kutoridhishwa na utendaji wa mahakama hiyo.
Nchi nyingine ambazo ziko katika mchakato wa kujitoa katika mahakama hiyo ni Afrika Kusini ambayo iliwasilisha barua yake ya kujitoa katika mahakama hiyo mwezi Machi mwaka jana na Gambia ambayo iliandika barua ya kujitoa mwezi Februari mwaka huo huo pia.


Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.