Huenda hii ndiyo ikawa sababu kwa baadhi ya wakulima nchini kulalamika wakikosa matokeo chanya katika kilimo licha ya kufuata kanuni zote zinazopaswa ikiwemo kupanda mbegu na kunyunyiza madawa kwa wakati lakini wakakwamishwa na ubora wa madawa ya viuadudu wanayonunua kutoka kwa wafanyabiashara wasio waaminifu waliozagaa maeneo mbalimbali nchini.
Taasisi ya udhibiti wa viuatilifu nchini(TPRI) imefanya msako katika maduka ya pembejeo za kilimo na mifugo mkoani GEITA na kubaini kuwepo kwa baadhi ya viuatilifu visivyo na ubora vinavyoingizwa nchini kwa njia za panya na kusababisha madhara kwa afya ya mimea na mifugo.
Katika
msako huo uliofanyika katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo,maafisa wa taasisi
wa TPRI wamelifunga duka la Msuka Agrovet lililoko Nyankumbu mjini Geita kwa
kuuza viuatilifu ambavyo havijafanyiwa utafiti,uchambuzi wala kusajiliwa na
taasisi hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.