ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, April 29, 2018

VIDEO JINSI ERASTO NYONI ALIVYOIUWA YANGA


Dakika 37 tu za kipindi cha kwanza zimetosha hii leo kuamua mshindi wa mchezo wa watani wa jadi wa Kariakoo baada ya mshambuliaji Erasto Nyoni kutumia vyema makosa ya mabeki wa Yanga na kuutupia mpira kambani kwa kichwa.

Simba imeibuka na ushindi wa goli 1-0 dhidi ya klabu ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Vodacom Tanzania Bara uliofanyika katika Uwanja wa Taifa leo Aprili 29, 2018 jijini Dar es salaam.
Hata hivyo mchezo huo ulionekana kuwa sawa kwa timu zote mbili kwani timu hizo zilionekana kushambuliana kwa zamu.

Kwa matokeo hayo Simba SC wameendelea kujiimarisha kileleni kwenye msimamo wa VPL kwa alama 62 wakifuatiwa na Azam alama 49 na huku Yanga wakisalia nafasi ya tatu kwa alama 48.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.