ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 9, 2018

KULA MIWA SAFI KWA AFYA YAKO

Miwa ina faida nyingi kiafya. Juisi ya miwa inafahamika na wataalamu wa afya kwa kuwa na uwezo wa kuupa mwili nguvu kwa sababu ya ‘glucose’ iliyopo.

Kijiko kimoja cha juisi ya miwa, kina kalori 11. Madini halisi na vitamin zinazopatikana katika sukari ni kama phosphorus, calcium, madini ya chuma na potassium.

Si hivyo tu, miwa ni jamii ya tunda lenye alkali hivyo lina uwezo wa kupambana na saratani hasa ile ya kibofu cha mkojo na saratani ya maziwa.

Miwa ina upekee wake kwani ina uwezo wa kuongeza maji mwilini, inaupooza mwili na kuupa nguvu.

Virutubisho vilivyopo katika miwa vina manufaa makubwa katika kusaidia utendaji kazi wa ogani muhimu kama figo, moyo, ubongo na viungo vya uzazi.

Pia, wagonjwa wa kisukari wasihofie sukari iliyopo kwenye miwa kwani haina madhara yoyote kwao. Uzuri wa juisi ya miwa ni kuwa sukari yake ni halisia.​ 

#mchakamchaka kwa hewa kupitia @jembefm #Mtonyo  #Buhongwa moja @prince_nzwalla @jimmykagaruki @deejaykflip

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.