ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, April 2, 2018

ACCOUNT YA HBABA YAWA HACKED, SASA YATUMIKA KUHAMASISHA MAANDAMANOG.SENGO TV
Mwanamuziki wa Bongo Fleva kutoka jijini Mwanza H. Baba amefunguka hii leo mara baada ya akaunti yake ya Instagram kudukuliwa (kuwa hacked)  na wajanja wenye nia ovu, ambapo pamoja na kuipokonya akaunti hiyo toka mikononi mwake na hata ashindwe kutupia picha zake au kujiachia na matukio mbalimbali kutokana na chaguzi lake, pia mtu/watu hao wamemstusha kwa posti ambazo zimekuwa ni zile za kuhamasisha maandamano yaliyo pigwa stop na jeshi la polisi nchini Tanzania kwa sababu za kiusalama ya tarehe 26/04/2018.

Kwa mujibu wa H. Baba amelalamika kuwa posti ya mwisho aliyoshuhudia jamaa hao wakiposti ni ile ya kuhamasisha wana Mwanza kukutana hiyo tarehe katika eneo fulani (......) katikati ya jiji la Mwanza na kisha taarifa ikaelezea ratiba nzima ya maandamano kwa mkoa.


Tayari taarifa zimefika kituo cha polisi Kirumba jijini Mwanza  kwa hatua za usalama. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.