Mwanamke mmoja kwa jina la Nishi Harishchandra Tripathi amefariki dunia na kumuachia mali zake zote nyota wa bollywood Sanjay Dutt.
Kwa mujibu wa habari,mwanamke huyo aliyekuwa akiishi Mumbai alifariki 15 mwezi Janauari baada ya kuugua.
Gazeti la Mumbai Mirror limeandika kuwa mwanamke huyo siku chache kabla ya kufariki kwake aliamua kumuachia mali zake zote muigizaji aliyekuwa akimpenda sana Sanja Dutt.
Sanjay Dutt alijawa na hisia baada ya kufahamishwa kuwa shabiki wake asiyemfahamu amefariki na kumuachia urithi wake wote.
Hata hivyo Sanjay Dutt amesema kuwa hawezi kuzikubali fedha hizo na kuwa mwanasheria wake tayari ameanza taratibu za kuuhamisha urithi huo kwa familia ya marehemu.
Nishi Harishchandra Tripathi alifariki akiwa na umri wa miaka 62.
Sanjay Dutt 58 ni kati ya nyota maarufu sana wa filamu za kihindi na ameshaigiza katika filamu zaidi ya 100.

Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.