Mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Simba SC dhidi ya Al Masry SC kutoka Misri, umemalizika usiku huu katika uwanja wa taifa kwa matokeo ya 2-2.
Walikuwa ni Simba walioanza kuziona nyavu za Al Masry mapema tu katika dakika ya 10 kwa nja ya penati, baada ya beki wao kuunawa mpira kwenye eneo la hatari.
Haikuchukua muda kwa Al Masry kusawazisha, kwani baada ya kufungwa bao la kwanza walianza mashambulizi makali langoni mwa Simba, na katika dakika ya 11, Ahmed alifunga bao la kusawazisha na kuufanya ubao wa matokeo uwe 1-1.
Mchezo huo ambao Al Masry waliutawala zaidi kipindi cha kwanza, mnamo dakika ya 26 tena walipata bao la pili kwa njia ya penati kupitia Abdalrauf, baada ya Erasto Nyoni kuunawa mpira ndani ya eneo la hatari.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Simba walikuwa nyuma kwa mabao 2-1.
Kipindi cha pili kilianza mwanzoni kwa Al Masry kuzidi kuonesha uhai, lakini baadaye Simba wakaanza kujibu mashambulizi wakilisakama lango la wapinzani wao, ambapo katika dakika ya 74, Emmanuel Okwi, aliweza kumlaza kwa chenga beki wa Al Masry na kuwa penati ambayo ilizaa bao la pili kwa Simba.
Mpaka kipyenga cha mwisho kinapulizwa, Simba SC 2-2 Al Masry SC.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.