Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika
shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari
2018. Picha Zote Na Mathias Canal
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikabidhi mifuko 20 ya saruji kwa ajili ya kuongeza nguvu katika ujenzi wa vyumba vya madarasa shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akichanganya udongo wakati akishiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018. Wengine (Kulia) aliyeshika jembe ni Mkuu wa Wilaya ya Mbeya Mhe Paul Ntinika na Kushoto ni Diwani wa Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles Mkera
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akipanga mawe kwenye msingi wa darasa ishara ya mafundi kuanza haraka ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akimpongeza Diwani wa Kata ya Iyera (CHADEMA) Mhe Charles Mkera kwa kushirikiana na serikali na kuhamasisha wananchi katika ushiriki wa ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya Sekondari Iyera wakati akiwa ziarani Mkoani Mbeya, Jana 2 Januari 2018.
Na Mathias Canal, Mbeya
Maendeleo ni mchakato wa kujenga jamii endelevu, yenye
kujiamini, kujituma na uwezo wa
kushiriki, kwa misingi ya usawa na kuheshimiana, katika kubuni, kuandaa na
kutekeleza mipango ya kujiletea “maendeleo” na kutumia matokeo ya kazi zao.
Naibu Waziri wa Wizara
ya Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa amekuwa mwalimu mzuri wa somo la Uraia Mkoani
Mbeya akifundisha kuhusu umoja na mshikamano huku akisisitiza kuwa Maendeleo ni
dhana pana kwa wananchi na hayapaswi kufanywa kwa mipaka ya vyama vya siasa.
Mhe Mwanjelwa ameyasema
hayo Jana 2 Januari 2018 wakati akizungumza na wananchi na mafundi wanaojenga majengo
ya Shule ya Sekondari Iyera ili kutatua changamoto ya kuwa na vyumba vingi vya
madarasa kwa ajili ya kuhimili wingi wa wanafunzi wanaotarajiwa kujiunga na
kidato cha kwanza mwaka huu.
Amewasisitiza mafundi
hao kujenga madarasa hayo kwa haraka na viwango vya hali ya juu kwani shule
zinatarajiwa kufunguliwa hivi karibuni huku shule hiyo ikiwa na upungufu wa
vyumba vinne vya madarasa.
Mhe Mwanjelwa alisema
kuwa tangu serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Mhe Dkt John Pombe Magufuli kutangaza utoaji elimu bure
kuanzia ngazi ya shule ya msingi hadi sekondari kumekuwa na ongezeko kubwa la
wananfunzi wanaojiunga na masomo ikiwa ni pamoja na kurejea shuleni kwa wananafunzi
waliokata tamaa ya kuendelea na masomo.
Alisifu juhudi za
Uongozi wa Wilaya ya Mbeya kwa kushirikiana kwa pamoja na wananchi katika shughuli
za maendeleo huku akiipongeza Halmashauri ya Jiji la Mbeya kwa kufanya vyema na
hatimaye kuongoza kwa ufaulu wa wanafunzi dhidi ya Halmashauri zingine za Mkoa
wa Mbeya.
Sambamba na hayo pia Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameongeza nguvu kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa katika shule hiyo ya Sekondari Iyera kwa kuchangia mifuko 20 ya saruji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.