Watu 36 wamefariki papo hapo na wengine 20 kujeruhiwa vibaya usiku wa kuamkia leo baada ya basi kuacha njia na kuporomoka kwenye kingo za fukwe ya Pasamayo nchini Peru.
Wizara ya afya nchini humo imesema mpaka kufikia sasa majeruhi 16 wapo katika hali mbaya huku wengine 4 wakiendelea na matibabu ya kawaida.
Tayari Rais wa nchi hiyo Pedro Pablo Kuczynski kupitia ukurasa wake wa Twitter ametoa salamu za rambi rambi kwa familia zilizopoteza ndugu zao.
Hata hivyo zoezi la uokoaji wa miili ya watu iliyokwama bondeni bado linaendelea kwa kutumia helikopita za kikosi cha Msalaba mwekundu.
Imeelezwa kuwa Babarara hiyo iliyo kando mwa habari ya Pacific ni moja ya barabara hatari zaidi nchini humo kwani kila mwaka wastani wa ajali tano hutokea.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.