Ajali hiyo ilitokea baada ya basi la abiria kugongana na lori katika barabara ya Nakuru – Eldoret nchini humo usiku wa kuamkia Desember 31, 2017.
Namnukuu President Magufuli ” “Nimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kutokea kwa ajali iliyosababisha ndugu zetu takribani 36 kupoteza maisha baada ya basi la abiria kugongana na lori,”
“Msiba huu umesababisha majonzi makubwa sio tu kwa ndugu zetu wa Kenya bali pia kwetu sote wana Jumuiya ya Afrika Mashariki, tumepoteza wapendwa wetu na nguvu kazi yetu.” – President JPM
“Kwa niaba ya Watanzania wote nakupa pole sana ndugu yangu Uhuru Kenyatta, Rais wa Jamhuri ya Kenya kwa msiba huu mkubwa ulioupata, nawapa pole wana familia wote waliowapoteza jamaa zao na pia nawapa pole wananchi wote wa Kenya.” – President JPM
“Naungana nanyi katika kipindi hiki kigumu cha majonzi, nawaombea majeruhi wote wa ajali hii wapone haraka na Marehemu wote wapumzishwe mahali pema peponi, Amina”. -President JPM
Hayo ndio maneno ya Rais Magufuli katika taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU Gerson Msigwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.