ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 4, 2018

CCM WILAYA YA GEITA WALAANI JESHI LA ZIMA MOTO KUWATOZA FEDHA KUBWA WACHIMBAJI BILA YA KUWAPATIA RISITI

Baadhi ya wachimbaji wa kijiji na kata ya Rwamgasa wakiendelea na kazi ya uchanjuaji wa madini ya dhahabu.

Moja kati ya wamiliki wa mialo ya uchenjuaji wa madini ya dhahabu akionesha risti ambayo sio ya EFD ambayo wamekuwa wakipatiwa baada ya kununua kifaa cha kuzimia moto.

Katibu mwenezi wa chama cha mapinduzi(CCM)Wilayani Geita Jonathan Masele akizungumza na wachimbaji baada ya kufika kwenye maeneo yao ya kazi na kukutwa baadhi ya makarasha yamefungwa na Jeshi la Zima moto na uokoaji.

Eneo la kuchenjulia dhahabu likiwa limefungwa na jeshi la zima moto na uokoaji.


Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi Wilayani Geita,Barnabas Mapande akikagua moja kati ya mtungi wa kuzimia moto wakati alipofika kuzungumza na kusikiliza changamoto za wachimbaji.

Kifaa cha kuzimia moto kikiwa kwenye eneo la kuchenjulia dhahabu.
Na,Joel Maduka,Geita.
Chama cha mapinduzi Wilayani Geita kimelaani kitendo cha jeshi la zima moto na uokoaji kuwatoza gharama kubwa  bila ya kuwapa stakabadhi za serikali  baadhi ya wachimbaji wadogo wa dhahabu kwenye kijiji cha Lwamgasa huku  wakifungiwa shughuli  za uchenjuaji madini hayo kutokana na baadhi yao kugoma kununua kifaa cha kuzimia moto.

Akizungumza baada ya kufika kwenye machimbo hayo na kujionea namna ambavyo wachimbaji hao wamefungiwa shughuli zao Katibu Mwenezi wa CCM Wilayani Humo Bw Jonatham Masele,amesema CCM imesikitishwa na jeshi la zima moto kuwatoza  Sh Lakini moja na elfu ishirini.

“Kiukweli sisi kama chama tumesikitishwa sanaa na kitendo cha jeshi la zima moto kuuza kwa bei kubwa bila ya kutoa risti mitungi hii ya gesi ya kuzimia moto na jambo jingine kuwafungia watu shughuli zao bila ya kuwapa elimu jambo hili sio nzuri tunaomba wajitahidi kuwaelimisha kwanza awa watu nasio kujichukulia hatua ya kuwafungia”Alisema Masele.

Bw Lehamu Lugiko , Mzee Mathew Kajoro  na Mwananyanzara Hamis wameelezea sababu kubwa ambayo imeendelea kuwapa mashaka wachimbaji kuwa ni kuuziwa mitungi ya kuzimia moto bila ya kupewa Elimu ambayo itawasaidia kupambana na majanga ya moto huku wakisikitishwa na kitendo cha kufungiwa kwa shughuli zao.

Mkuu wa Jeshi la zimamoto na uokoaji  Mkoani Geita Bw Elisa Mgisha amesema wao sio wasambazaji kwani kuna watu ambao ni mawakala na kwamba suala la risti za EFD inatokana na wafanyabiashara wenyewe na kuhusu kuuziwa kwa bei kubwa ni kwamba wao wanapotoa kibari cha mawakala yeye ndiye mwenye jukumu la kupanga bei ya kuuza mtungi vile ambavyo anaonelea.


Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Geita Bw Barnabas Mapande amemtaka mkuu wa jeshi la zima moto kushughulikia tatizo hilo na kuacha kuendelea kuwakandamiza wananchi na wafanyabiashara pindi wanapokuwa kwenye shughuli zao za kujitafutia kipato.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.