ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, January 4, 2018

HIKI NDICHO KILICHO MSUKUMA WAZIRI MWAKYEMBE KUJA NA AGIZO KWA TFF.



Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma yanapaswa kutizamwa kwa dhati kwani nyuma yake mathalani kwa mchezo wa Dodoma Fc v Alliance kwa mujibu wa mwanahabari Juma Ayoo wa Jembe Fm anasimulia yale yaliyojiri dimbani kabla ya tamko la Waziri mwenye dhamana ya michezo Dkt. Harrison Mwakyembe kuitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, ili kuhakikisha utata unamalizika.

TAMKO LA WAZIRI. 
MWAKYEMBE ATOA MAAGIZO MAZITO TFF 
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Harrison Mwakyembe ameitaka TFF kuyafanyia kazi malalamiko yote yanayohusu michezo ya ligi daraja la kwanza, kati ya Dodoma FC vs Alliance na Pamba vs Biashara.

Sakata la maamuzi yasiyo ya haki katika michezo ya Dodoma FC dhidi Alliance ya Mwanza na Pamba ya Mwanza dhidi Biashara ya Musoma ndio limefanya Waziri mwenye dhamana ya michezo kutoa agizo hilo kwa shirikisho ili kuhakikisha utata huo unamalizika.

Katika taarifa yake  Waziri Mwakyembe ameeleza kusikitishwa na malalamiko ya vitendo vya uonevu na upendeleo katika maamuzi ya mechi hizo huku TFF ikiwa kimya bila kutoa ufafanuzi wa maamuzi hayo.

Mechi hizo zilipigwa Disemba 30 maamuzi yake kugubikwa na utata mkubwa hivyo Waziri amemtaka Rais wa TFF Wallace Karia na viongozi wengine wahusika kuchukua hatua za kuchunguza maamuzi hayo na kuchukua hatua.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.