ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, December 8, 2017

HABARI YA UZINDUZI WA WIKI YA NENDA KWA USALAMA MKOA WA GEITA.

Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa  koti la rangi ya dhambarau na miwani akipata maelezo juu ya matumizi ya kamera za barabarani kutoka kwa Inspekta wa Usalama barabarani Mkoa wa Geita Mark Thomas Masawe wakati wa ukaguzi wa mabanda ya maonyesho katika maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani Mkoani Geita.
Mtaalam wa Mamlaka ya udhibiti wa usafiri wa nchi kavu na Majini (SUMATRA) ndugu Hagai Ruben akitoa maelezo kuhusu ukataji wa leseni za usafirishaji kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani iliyofanyika kimkoa Katoro Geita.
Wataalam wa Jeshi la Zima Moto na Wokozi Mkoa wa Geita wakieleza mbele ya wajumbe wa baraza la usalama barabarani  Mkoa wa Geita matumizi mbalimbali ya mitungi yenye Gesi ya kuzima moto baada ya kamati hiyo kutembelea banda la kikosi hicho.

Ndugu Emmanuel Chacha mtaalam kutoka kampuni ya uchimbaji wa madini Geita (GGML) akitoa ufafanuzi  kwa Mkuu wa Mkoa wa Geita na wajumbe wa baraza la Usalama barabarani kuhusu matumizi ya vifaa vya wokozi katika maeneo ya migodi.
Wanafunzi wa Shule za Msingi za Mji wa mdogo wa Katoro wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
Maandamano ya maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa usalama barabarani yakipita mbele ya Mgeni rasmi (hayupo kwenye picha).
Waendesha Piki Piki maarufu kama boda boda wakiwa katika maandamano ya maadhimisho ya wiki ya nenda kwa usalama barabarani iliyofanyika Katoro Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita akimpongeza ndugu Alfred Hussein Mkuu wa Kikosi cha Usalama barabarani Mkoa wa Geita wakati wa maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.

Mkuu wa Mkoa wa Geita Robert Gabriel akihutubia wananchi(awapo katika Picha) wakati wa wa uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita Mponjoli l.Mwabulambo akizungumza akitoa maelezo baada ya uzinduzi wa maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa Usalama barabarani Mkoani Geita.
PICHA ZOTE NA: Magesa Jumapili

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.