Hospitali hii ndiyo imebaki pekee kama tegemeo la wakazi wote wa vijiji vinavyoizunguka wilaya ya Sengerema. |
WANANCHI WAKAZI WA
KIJIJI CHA ISENYI KATA YA NYAKASASA KISIWA CHA KOME WILAYANI SENGEREMA
WAMEIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUMALIZIA UJENZI WA ZAHANATI ILI KUWAONDOLEA KERO
YA KUTEMBEA KWA UMBALI MREFU KWEMDA KIJIJI JIRANI KUTAFUTA HUDUMA YA AFYA
Wakizungumza na JEMBE
FM wakazi hao wamesema kuwa wamekuwa wakiangaika na wakitembea umbali mrefi
kwenda cliniki kijiji jirani kupata
huduma ya afya na kusababisha baadhi ya akina mama kuzalia njiani na wengine
kupoteza maisha hasa nyakati za usiku.
Kwa upande wake mwenyekiti waserikali ya kijiji hicho
cha ISENYI bwana VEDASTUSI ITOBI amekiri
kuwepo kwa kero hiyo ambayo ni miaka saba tangu kuanza kwa ujenzi wa zahanati
hiyo na kuongeza kuwa wamekuwa wakipewa wakipewa
ahadi na baadhi ya viongozi lakini hazitimiliziki. BOFYA HAPA KUSIKILIZA.
Ili kukamilisha ujenzi wa zahanati hiyo Mwenyekiti huyo
amesema wananchi waneshasomba mawe na mchanga changamoto kuwa nikiwa ni fedha
ya kuwalipa mafunzi na kuiomba serikali kuwasaidia kukamilisha ujezi wa
zahanati hiyo ili kuwaondolea adha wananchi kijijini hapo
Endapo Zahanati hiyo itakamilika na kuwanza kutoa huduma ya
afya zaidi ya kaya 1200 zifanufaika na huduma.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.