Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa nne
kutoka kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mawaziri kutoka Uganda mara baada
ya kuwasili kwenye Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili
kushoto) na Waziri wa
Nchi anayeshughulikia Madini wa Uganda, Lokeris Peter
(kushoto) wakitembelea mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo Rwamgasa. Wa pili
kutoka kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Geita, Mhandisi Robert Lughumbi na kulia ni
mmiliki wa mgodi huo, Christopher Kadeo.
Mawaziri kutoka Uganda
wakimsikiliza mmiliki wa Mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef, Christopher Kadeo
(hayupo pichani) baada ya kutembelea eneo (shimo) linalochimbwa Dhahabu. Kutoka
kushoto ni Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga
Kania, Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi, Dkt. Kasirivu Atwooki, Waziri wa
Nchi- Madini, Lokeris Peter na Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji Mkuu wa Kampala,
Namugwanya Bugembe.
Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo (kulia)
akiongozana na Waziri wa
Nchi anayeshughulikia masuala ya Madini nchini Uganda, Lokeris Peter (kulia
kwake) mara baada ya kuwasili kwenye Mgodi wa
Dhahabu wa Busolwa Gold Mine Project uliopo Nyarugusu.
Mawaziri kutoka Uganda wakiwa pamoja na mwenyeji
wao, Naibu Waziri wa Madini, Stanslaus Nyongo walipotembelea mgodi wa Dhahabu
wa Blue Reef uliopo Rwamgasa ili kujionea shughuli zinavyoendeshwa mgodini
hapo.
Waziri wa
Nchi anayeshughulikia masuala ya Madini nchini Uganda, Lokeris Peter (kushoto)
akiongozana na wenyeji wake, Naibu Waziri wa
Madini, Stanslaus Nyongo (wa pili kutoka kushoto) na Mkuu wa Mkoa wa Geita,
Mhandisi Robert Lughumbi walipotembelea mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo
Rwamgasa.
MAWAZIRI WA UGANDA WATEMBELEA MIGODI YA WACHIMBAJI
WADOGO GEITA
Mawaziri
Wanne kutoka Uganda wakiongozwa na mwenyeji wao Naibu Waziri wa Madini,
Stanslaus Nyongo Agosti 29, 2017 walitembelea migodi ya dhahabu ya Mkoani Geita
inayomilikiwa na Watanzania.
Miongoni
mwa migodi iliyotembelewa ni Mgodi wa Dhahabu wa Blue Reef uliopo Rwamgasa,
Mgodi wa Dhahabu wa Busolwa Gold Mine Project uliopo Nyarugusu na Kituo cha
Mfano cha Uchimbaji Madini ya Dhahabu cha Tan Discovery kilichopo Rwamgasa.
Mawaziri
hao waliwasili nchini Tanzania Agosti 27, 2017 kwa ajili ya zira ya siku mbili
ya kujifunza juu ya Usimamizi wa Sekta ya Madini hususan suala la Uendelezaji
wa Uchimbaji Mdogo wa Madini.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri Nyongo, Mawaziri hao
wametembelea migodi hiyo ili kuona namna gani migodi hiyo inaendesha shughuli
zake na namna ambavyo serikali imekuwa ikiwasaidia kuhakikisha wanakuwa na
uchimbaji madini wenye tija.
“Wamekuja
kujifunza, kuangalia Sera zetu, Sheria zetu na mchango wa Serikali katika
kuwasaidia wachimbaji wadogo,” alisema.
Alisema
walipendekeza kutembelea migodi inayomilikiwa na Watanzania ili kujionea namna ambavyo
wazawa wanavyoendesha shughuli za uchimbaji madini ikiwa na pamoja na
kuzungumza nao ili kupata uzoefu wa uendeshaji wa shughuli husika na kubaini
ushirikiano uliopo baina yao na Serikali.
Akizungumza kwa niaba ya Mawaziri wa
Uganda, Waziri wa Nchi anayeshughulikia Madini wa Uganda, Lokeris Peter alisema
Tanzania ni miongoni mwa nchi Barani Afrika zilizopiga hatua kwenye usimamizi
wa Sekta ya Madini hususan eneo la Uchimbaji Mdogo wa Madini ikilinganishwa na
nchi zingine walizotembelea.
"Uamuzi
wa kufanya ziara nchini humu unafuatia uzoefu wa muda mrefu wa Tanzania kwenye
masuala ya uchimbaji wa madini hususan namna ambavyo Tanzania imeweza kurasimisha
suala la uchimbaji mdogo," alisema Waziri Peter.
Awali
kabla ya kuwasili Mkoani Geita, ujumbe huo wa Mawaziri kutoka Uganda; Agosti
28, 2017 ulikutana na Waziri wa Madini, Angellah Kairuki ambapo ulielezwa
masuala mbalimbali yanayohusu sekta husika ikiwemo Sera, Sheria
na Kanuni za Madini pamoja na masuala yanayohusu Wachimbaji Wadogo wa madini.
Mawaziri
kutoka Uganda waliofanya ziara hiyo ni Waziri wa Nchi- Madini, Lokeris Peter,
Waziri wa Nchi- Mambo ya Ndani, Obiga Kania, Waziri wa Nchi- Mamlaka ya Mji
Mkuu wa Kampala, Namugwanya Bugembe na Waziri wa Nchi- Masuala ya Uchumi,
Dkt. Kasirivu Atwooki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.