Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa wa Geita aliyevaa miwani na Koti
la kijivu akimpokea Waziri wa Madini wa Uganda Mheshimiwa Lokeris Peter
baada Mkoani Geita na ujembe wa Mawaziri wanne na wanasheria kwa ajili
ya kujifunza namna Serikali ya Tanzania inavyowawezesha wachimbaji wadogo, Kati
na Wakubwa katika Shughuli zao.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo Mwenye kizibao cha
rangi nyukundu akiwa na viongozi wa Mkoa wa Geita pamoja na Mawaziri wanne wa
Serikali ya Uganda baada ya Kuwasili Mkoani Geita kujifunza uchimbaji mdogo,
Kati na Mkubwa wa Madini.
Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhandisi Robert Gabriel wa kwanza kulia
akiwaongoza Mawaziri kutoka Uganda kwenda kukagua shughuli za uchimbaji mdogo
Lwamgasa Wilayani Geita.
Mawaziri wanne kutoka kutoka Uganda pamoja na viongozi wengine wa
Wizara ya Madini na Mkoa wa Geita wakujionea shughuli za ujenzi wa Kituo cha
mfano cha Serikali zinavyoendelea katika eneo la Lwangasa Wilayani Geita. Kituo
hiki kinajengwa kwa ajili ya kutoa mafunzo kwa wachimbaji wadogo wa madini ya
Dhahabu.
Naibu Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo akiongozana na
Mawaziri kutoka Uganda pamoja na wataalamu wa Madini kukagua shughuli za
uchimbaji mdogo wa madini katika mgodi wa Kadeo Lwamgasa Geita.
Mmiliki wa Mgodi wa KADEO Mine Limited ndugu Kadeo akitoa maelezo kwa
Mawaziri na wataalmu wa madini walipotembelea Mgodi wa KADEO Mine kujifunza
shughuli za uchimbaji mdogo wa Dhahabu Kata ya Lwamgasa Geita.
Mhandisi Robert Gabriel Mkuu wa Mkoa Geita mwenye koti la kijivu na
miwani akiwaongoza Mawaziri kutoka
Uganda kukagua shughuli za uchimbaji wa madini katika mgodi wa KADEO.
Naibu
Waziri wa Madini Mheshimiwa Stanslaus Nyongo akizungumza na wadau wa
madini na wanachama wa chama cha wachimbaji wadogo wa madini katika
Mgodi wa Busolwa Mine wakati wa zaiara ya mwaziri waane kutoka Uganda ya
kujifinza uchimbaji mdogo wa Madini.
Mwaziri
kutoka nchini Uganga pamoja na wataalamu wa madini wakifuatilia kwa
karibu shughuli za uchimbaji mdogo zinavyofanyika katika Mgodi wa KADEO
Limited uliopo kata ya Lwamgasa walipokwenda kujifunza uchimbaji Mdogo.
PICHA ZOTE NA Magesa Jumapili Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Geita
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.