ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 13, 2017

"MASIKINI" LULU SASA JELA MIAKA MIWILI.



BREAKING: Jaji Sam Rumanyika amemkuta na hatia msanii Elizabeth Michael ya kumuua bila kukusudia msanii Steven Kanumba, na kumhukumu kwenda jela miaka miwili - 

 " Hata kama marehemu angefufuka kwa miujiza Mahakama hii haitaweza kuchukuwa ushahidi wake" amesema jaji.

Naye wakili msomi wa mwigizaji huyo, Mhe. Peter kibatala amesema anashughulikia rufaa ili mteja wake apunguziwe adhabu. 


LULU AHUKUMIWA KWENDA JELA MIAKA MIWILI KWA KUMUUA MSANII MWENZAKE STEVEN KANUMBA BILA KUKUSUDIA
Mahakama Kuu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imemhukumu KWENDA JELA MIAKA MIWILI MUIGIZAJI WA BONGO MOVIE Elizabeth Michael "Lulu" ambaye alikuwa anakabiliwa na KESI YA KUUA BILA KUKUSUDIA.

Hukumu hiyo imetolewa leo November 13, 2017 na Jaji Sam Rumanyika aliyekuwa anaendesha kesi hiyo, na kusema kwamba mshtakiwa amekutwa na hatia ya kuua bila kukusudia kutokana na ushahidi wa mazingira, hivyo atatumikia kifungo cha miaka miwili jela.
#Nukuu…Ya Jaji Rumanyika...Hapa Chini.


"Ushahidi wa mazingira unaweza kutumika kama msingi pekee wa kumtia hatiani mshtakiwa tena mshtakiwa pekee, sasa ninapokwenda kuangalia maelezo ya mshtakiwa kama yanakidhi vigezo nilivyosema awali, kwa mujibu wa mshtakiwa alisema alianza kupigwa na marehemu, marehemu alilewa lakini kuhusu mshtakiwa anatakiwa kutoa maelezo yanayo jitosheleza, kwa hili mshtakiwa alijikanganya" amesema Jaji Rumanyika.


Jaji Rumanyika ameendelea kwa kusema kwamba.."mshtakiwa katika maelezo yake hakueleza kuwa marehemu alianguka au laah wakati anamkimbiza, maelezo ya Dkt. Josephine siyo maelezo ya cheti cha hospitali, hayakuwa na hadhi ya hospitali".


"Inakinzana na hekima ya kawaida kwamba hata pale marehemu alipoendelea kumpiga na kumshambulia na akaenda kiwango cha kumtishia kumuua, mstakiwa hakuthubutu hata kumpiga, ina maana alifanya kama maneno ya biblia yanavyosema mtu akikupiga shavu la kushoto mgeuzie na la kulia lakini hili mshtakiwa hakulisema.", amesema Jaji Rumanyika.


"Na wakati huo mshtakiwa alikuwa na miaka 17, leo ana miaka 22, alikuwa mtoto hivyo asingetambua kuwa kinachofanyika ni kibaya au kizuri, huyu mtoto sio mshtakiwa aliyelengwa nasheria ya watoto, kama mtoto wa umri huu na anaweza kafanya ya watu wazima, mahakama hii haikubaliani bali mshtakiwa ni mkomavu, hakuna mashaka kuwa kifo cha marehemu kilitokana na ugomvi", ameendelea kusema Jaji Rumanyika mahakamani hapo.


Baada ya hapo jaji rumanyika aliwapa nafasi upande wa mshtakiwa kujitetea ambapo wakili wake Peter Kibatala alimtetea mshakiwa kwa kusema kuwa mshtakiwa anategemewa na familia yake.
Baada ya hapo Jaji Rumanyika alitoa hukumu yake na kumuamuru mshtakiwa kwenda jela kwa miaka miwili.


Elizabeth Michael (Lulu) anahukumiwa kwa kumuaa aliyekuwa mpenzi wake Steven Charles Kanumba ambaye pia ni muigizaji mwenzake, mnamo April 7, 2012.


BOFYA HAPA KUSIKIA NI WAFUNGWA WENYE MAKOSA AINA GANI HUNUFAIKA NA MSAMAHA WA RAIS KUPITIA UDUKUZI ULIOCHOMOZA NDANI YA KAZI NA NGOMA.
........

#KAZINANGOMA @mansourjumanne @gsengo @DjScorpion

Picha na Kajuna. 

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.