Jaffo- “Mabilioni Kwa Afya za Watanzania”
Na. Atley Kuni- TAMISEMI
Serikali
imepanga kukarabati vituo vya afya 172 kutokana na fedha kutoka Benki ya Dunia
na Ubalozi wa Canada ambapo wametoa jumla ya Dolla za Kimarekani Mil 88
sambamba na Bil.12 fedha za kitanzania zilizovuka katika mwaka wa fedha wa
2016/2017.
Naibu
Waziri wa Nchi Ofisi Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mh. Seleman Jafo
(Mb) amesema lengo la serikali nikuhakikisha ifikapo Desemba 30, 2017 shughuli
hiyo iwe imekamilika ipasavyo kwa kusimamiwa karibu na Waheshimwa Wakuu wa
mikoa wakisaidiana na Waheshimiwa Wakuu wa Wilaya.
Jafo
amesema kupitia Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Serikali imepokea Dolla za
kimarekani Mil. 66 kutoka Benki ya Dunia
ambapo vituo 103 vitakarabatiwa aidha pia Serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI, imepata
Msaada kutoka Ubalozi wa Canada wa dolla za kimarekani Mil 22, ambapo vituo 44
vya afya vitakarabatiwa kwa fedha hizo.
Naibu
waziri huyo alisema, fedha zingine
zitakazo tumika katika zoezi hilo ni zile zilizo vuka katika mwaka wa fedha
uliopita.
“Vituo
25 vitafanyiwa ukarabati kupitia fedha za Benki ya Dunia na mfuko wa afya wa
pamoja zilizovuka mwaka wa 2016/2017, ambapo Bil.12 za kitanzania zitatumika,”
alisema Jafo na kuongeza kwamba
kila “kituo kitapatiwa shilingi Mil. 500
za kitanzania na baada ya ukarabati serikali itakuwa na jukumu lakupeka vifaa
katika maeneo hayo”.
Waziri
Jafo amesema, Maeneo ya kipaumbele wakati wa ukarabati huo ni pamoja na Upasuaji (Theater), Wodi za mama na Mtoto
(Martenity), Maabara(Laboratory), pamja na Nyumba za watumishi sambamba na
maeneo mengine ya kipaumbele kutokana na fedha zilizopo.
Katika
hatua nyingine Jafo amewagiza Makatibu Tawala wa mikoa kuwasilisha Taarifa ya
kila mwezi ofisini kwake juu ya maendeleo ya ukarabati, huku akiwataka
Wakurugenzi na watendaji wengine kusimamia kwa ufasaha zoezi hilo.
Naibu
Waziri hakusita kuonya juu wale wote watakao kwenda kinyume na maagizo na
maelekezo ya serikali yaliyotolewa.
“Nawaomba
Wah. Wabunge na Madiwani kushirikiana
bega kwa bega na watendaji katika kufanikisha zoezi hili kwa ufanisi, alisema
Jafo na kuongeza kwamba, “ofisi yangu
haita mvumilia Kiongozi au Mtendaji yeyote atakaye onekana kutumia fedha hizo
vibaya au kushindwa kutimiza wajibu wake na kisha kukwamisha shughuli hii
muhimu yenye nia njema kwa maisha ya watanzania.
Akihitimisha
maagizo hayo Naibu waziri Suleima Jafo,
amezishukuru Wizara zote za kisekta
katika kusukuma gurudumu la maendeleo na
kwenda sambamba na kasi ya Rais Mh. Dkt.
John Pombe Magufuli ya HAPA KAZI TU, ikiwapo, Wizara ya Afya, Fedha na Mipango
pamoja na watendaji wa Ofisi yake ambao walikuwa bega kwa bega katika mchakato
wote wa kupatikana kwa fedha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.