NA ZEPHANIA MANDIA
Mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA ameanza jitihada za kuhakikisha anapunguza kama siyo kumaliza kabisa migogoro ya ardhi katika jiji la mwanza na manispaa ya Ilemela, maeneo ambayo kwa muda mrefu yamegubikwa na migogoro ya ardhi.
Jitihada hizo zimeanza katika Manispaa ya Ilemela na jiji la Mwanza ambako akiwa amefuatana na wataalam wa halmashauri ameweza kuhudumia mamia ya wanachi ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakizungushwa bila ya kupata haki zao.
Mamia ya wananchi kutoka nyamagana na Ilemela baadhi yao wakiwa wamedhoofu kwa uzee na mahangaiko ya muda mrefu kutokana na kufuatilia haki ya ardhi waliyokuwa wakimiliki katika halmashauri, bila ya mafanikio. Hata hivyo Jitihada zilizoanzishwa na mkuu wa mkoa wa Mwanza JOHN MONGELA za kutafuta ufumbuzi zimerejesha tabasamu kwa wazee waliohangaika kwa zaidi ya miaka 20.
Wataalamu kitengo cha ardhi katika manispaa ya Ilemela na jiji la Mwz walikuwa na wakati mgumu kutoa majibu ya kero za wananchi.
ENGBERT REBUKABWE – MTHAMINI ARDHI Akaonja shubiri ya MONGELA ambaye ni mkuu wa mkoa wa Mwanza.
Mwanza JOHN MONGELA amefanyakazi kwa zaidi ya saa 18 hadi saa sita usiku akisuluhisha migogoro ya ardhi katika manispaa ya Ilemela na siku iliyofuata amekuwa ktk wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.